Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-Siasa-Usalama

Mashambulizi ya jeshi la Israel yanaendelea katika ukanda wa Gaza

Mashambulizi ya jeshi la anga la israeli katika mji wa Gaza yameingia siku ya nne leo ijumaa katika operesheni serikali ya Israeli inayodai kwamba ni kukabiliana na kundi la Hamas kwa lengo kulishawishi lisitishe harakati zake za kurusha makombo katika aridhi ya Israel.

Mitambo ya kijeshi ya Israel imedhibiti kwa asilimia 90 makombora yanayorushwa kutoka nchini Palestina.
Mitambo ya kijeshi ya Israel imedhibiti kwa asilimia 90 makombora yanayorushwa kutoka nchini Palestina. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo na hasara nringine vinaendelea kuongezeka kutokana na mashambulizi hayo katika aridhi ya Palestina, huku jumuiya ya kimataifa ikijitahidi kwa namna moja ama nyingine kushawishi Israeli na kundi la Hamas kusitisha mapigano.

Watu wanaendelea kupoteza maisha katika ukanda wa Gaza.
Watu wanaendelea kupoteza maisha katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Majdi Fathi

Marekani imesema iko tayari kusaidia upatikanaji wa suluhu kati ya Israel na wapiganaji wa Kipalestina wa Hamas. Rais Barrack Obama amempigia simu waziri mkuu wa Isreali Benjamin Netanyahu na kumhakikishia hilo wakati huu jeshi la Israel likiendelea kushambulia ngome za Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Hata hivyo, Netanyahu alinukuliwa akisema mashambulizi hayo yataendelea kama ilivyopangwa wakati ambapo kundi la Hamas litakua likiendelea na harakati zake za kurusha makombora yake katika ardhi ya Israel.

Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel yanaendelea kusababisha hasara katika ukanda wa Gaza..
Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel yanaendelea kusababisha hasara katika ukanda wa Gaza.. ©Reuters.

Tangu kuanza kwa mashambulizi hayo katika ukanda wa Gaza, zaidi ya watu 90 wamepoteza maisha katika eneo hilo lakini Israel imesema hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha. Ron Prosor balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa, amelimabia baraza la usalama jijini New York kuwa, kundi la Hamas limeendela kurusha maroketi licha ya jeshi la nchi yake kujizuia kutekeleza mashmabulizi zaidi.

Naye Riyadh Mansour Balozi wa Palestina katika Umoja huo ameishtumu Israel kuendelea kutekeleza mashambulizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.