Pata taarifa kuu
UNSC-GAZA-ISRAELI-HAMAS-Mapigano

Jitihada za UNSC kwa kusitisha mapigano Gaza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa likiandaa kikao cha dharura kujadili makabiliano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Watu zaidi ya 500 wauawa Gaza, na jeshi la Israeli ladai kupoteza wanajeshi wake 13 katika mashambulizi yanayoendelea.
Watu zaidi ya 500 wauawa Gaza, na jeshi la Israeli ladai kupoteza wanajeshi wake 13 katika mashambulizi yanayoendelea. REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Ukanda wa Gaza unaendelea kukumbwa na mtiririko wa mabomu, huku raia wa kawaida wasiyokua na hatia hususana watoto wakiendelea kufariki. Zaidi ya wapalestina 500 wameuawa katika mashambulizi haya ya jeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza, huku Israel ikisema wanajeshi wake 13 wamepoteza maisha.

Watoto wanaendelea kuuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza.
Watoto wanaendelea kuuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Suhaib Salem

Shirika la watoto Unicef limeelezea masikitiko yake kuona watoto watoto ndio wanalengwa katika mashambulizi hayo.

Jumapili wiki iliyopita mtaa wa Chajaya, mashariki mwa Palestina, umeshuhudia mashambulizi yaliyosababisha maafa makubwa, ambapo watu takribani 73 wameuawa. Kwa siku nzima ya Jumapili jana watu 120 wameuawa.

“Idara za huduma za dharura zinakabiliwa na wingi wa majeruhi. Baadhi wamelazwa kwenye sakafu na wengine kwenye viti, na kuna wengine ambao wamejazana kwenye vitanda, hatuna namna nyingine ya kufanya” , Mkurugenzi wa hospitali za Gaza, abelattif Al Haj, ameiyambia RFI Jumapili jana.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajaribu kutafuta mwafaka wa namna ya kusitisha mapigano yanayoendelea na hadi sasa haijabanika ni kitu gani walichoafikiana.

Palestina kupitia balozi wake katika Umoja wa Mataifa Riyadh Mansur amelihstumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutochukua hatua za kusitisha operesheni ya Isreal.

Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israeli yaendelea kusababisha vifo Gaza.
Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israeli yaendelea kusababisha vifo Gaza. REUTERS/Suhaib Salem

Naye balozi wa Israel katika Umoja huo, Ron Prosor amesema jeshi la Israel litaendelea na operesheni hiyo hadi pale kundi la Hamas litakapoacha kurusha maroketi katika ardhi yake.

Waziri wa mambo nje wa Marekani John Kerry anawasili jijini Cairo nchini Misri leo Jumatatu kusaidia jitihada za kupatikana kwa mwafaka wa kusitisha makabiliano yanayoshuhudiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.