Pata taarifa kuu
SYRIA-KOBANE-IS-MAPIGANO-USALAMA

IS yapoteza mji wa Kobane

Waasi wa Islamic State wameondolewa katika mji wa Kobane nchini syria na wapiganaji wa Kikurdi.

Mapigano yakirindima katika mji wa Kobane, Oktoba 29 mwaka 2014.
Mapigano yakirindima katika mji wa Kobane, Oktoba 29 mwaka 2014. REUTERS/Yannis Behrakis
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo wa kijeshi nchini Syria uliotangazwa na msemaji wa wapiganaji wa kikurdi Polat Can unakuja sanjari na ushindi mwingine wa nchini Iraq ambapo afisa mmoja wa kijeshi ametangaza kukombolewa kwa jimbo la Diyala mashariki mwa nchi hiyo kutoka utawala wa kundi la wapiganaji wa la Dola la Kiislam.

Mapema Jumatatu wiki hii, shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria (OSDH) limetangaza kudhibitiwa kwa asilimia mia moja kwa mji huo wa Kobane ulioko mpakani na nchi jirani ya Uturuki na ambao hadi sasa umekuwa ishara ya upinzani dhidi ya Kundi la Dola la kiislam ambapo wanajihadi hao walianzisha mashambulizi Septemba 16 mwaka 2014.

Aidha, Katika maeneo kadhaa ambayo ni ya kikurdi nchini Syria, umati wa waliingia mitaani kusherehekea ushindi huo, huku mjini Paris, nchini Ufaransa watu wasiopungua 300 wamekusanyika kwenye eneo la Jamhuri “Place de la Republique”, na kupeperusha bendera ya Kikurdi na mabango, huku muziki wa jadi ukirindima.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ambayo mapema siku ya Jumatatu imechukua tahadhari ya kutothibitisha udhibiti wa asilima mia moja wa mji wa Kobane ikizungumzia asilimia sabini tu, hatimaye imetangaza kuwa vikosi vya Kikurdi vimeudhibiti mji wa Kobane kwa asilimia tisini baada ya mapambano yaliyodumu kwa takriban miezi minne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.