Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-SHAMBULIZI

Afghanistan: shambulio la kujitoa mhanga Jalalabad

Mashariki mwa Afghanistan, watu wasiopungua 14 wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga lililotekelezwa wakati wa kikao cha viongozi wa makabila "Jirga", nyumbani kwa diwani wa serikali za mitaa katika mji wa Jalalabad.

Askari wa Afghanistan waliotumwa kwenye eneo la shambulio, Januari 17 2016.
Askari wa Afghanistan waliotumwa kwenye eneo la shambulio, Januari 17 2016. Noorullah Shirzada / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Taliban limekana kuhusika na shambulio hilo, wakati ambapo kundi la Islamic State halijatoa taarifa yoyote kuhusina na tukio hilo.

Shambulio hilo limetokea Jumapili hii nyumbani kwa diwani wa serikali za mitaa katika mji wa Jalalabad, mji mkubwa wa mashariki mwa Afghanistan. "watu wengine 13 [wamejeruhiwa] ", ofisi ya mkuu wa mkoa wa Nangarhar imebaini. Jalalabad ni mji mkuu wa mkoa wa Nangarhar. Idadi ambayo imethibitishwa na Najibullah Kamawal, mkurugenzi wa huduma za afya katika mkoa huo.

Akihojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, Zabiullah Mujahid, msemaji wa kundi la Taliban, amehakikisha kwamba wapiganaji wa kundi hilo hawahusiki kamwe na shambulio hilo, ambalo linatokea siku moja kabla ya mkutano mjini Kabul unaolenga kufufua mazungumzo ya amani kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan. Mazungumzo ambayo yalisimamishwa tangu majira ya joto mwaka uliyopita. Kundi la Islamic State ambalo lilitekeleza shambulio juma lililopita dhidi ya ubalozi mdogo wa Pakistan katika mji wa Jalalabad, hadi sasa, halijakiri kuhusika na tukio hilo.

Ongezeko la mashambulizi

Shambulio hilo limetokea wakati wa kikao cha viongozi wa makabila (Jirga), nyumbani kwake Ubaidullah Shinwari, diwani wa serikali za mitaa katika mkoa Nangarhar. Afisa huyo hakupata jeraha lolote, lakini nduguye na baba yake wamejeruhiwa.

Kuongezeka kwa mashambulizi nchini Afghanistan na askari wa serikali kurejeshwa nyuma na wapiganaji wa Taliban, ambao walivamia na kuuteka kwa muda wa siku tatu mji wa Kunduz (kaskazini mwa Afghanistan) mwezi Septemba, vinaambatana na juhudi za kufufua mchakato wa amani kati ya serikali ya Kabul na wapiganaji wa Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.