Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-USALAMA

Syria: kundi la IS laanza kuondoka kusini mwa Damascus

Maafisa kadhaa na wapiganaji wa kundi la Islamic State pamoja na familia zao wameanza kuuhama wiki hii, maeneo ya Qadam al-Hajar al-Aswad, kusini mwa jimbo la Damascus. Wanaelekea katika mji wa Raqqa, mji mkuu uliotangazwa na kundi la hilo. Mamia zaidi wanatarajiwa kuendelea zoezi hilo katika siku zijazo.

Wakazi wa mji wa Qadam wakisubiriwa katika mji wa Damascus ili waweze kurejea katika makazi yao, walioyakimbia kutokana na mapigano ya waasi, Jumatano, Januari 20, 2016.
Wakazi wa mji wa Qadam wakisubiriwa katika mji wa Damascus ili waweze kurejea katika makazi yao, walioyakimbia kutokana na mapigano ya waasi, Jumatano, Januari 20, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano ya kuhuma maeneo ya kusini mwa jimbo la Damascus yaliafikiwa katikati ya mwezi Desemba kati ya waasi wenye silaha na serikali ya Syria. Makubaliano haya yanahusu hasa wapiganaji wa kundi la Islamic State pamoja na wale wa kundi la al-Nosra Front, tawi Al Qaeda nchini la Syria. Lakini utekelezaji wake ulisitishwa baada ya kifo cha kiongozi wa waasi Zahran Allouche, aliyeuawa Desemba 25 katika mashambulizi ya anga ya Syria.

Mapema wiki hii, mkataba huo ulirudi kutekelezwa. Maafisa wa kundi la IS, wapiganaji wa kundi hili na familia zao walikuwa wa kwanza kusafiri kwa basi, huku wakikataa kuzungumza lolote kwa vyombo vya habari. Wanachama hao wa kundi la Islamic State wameelekea katika mji wa Raqqa, mji mkuu wa kundi hilo kaskazini mwa Syria. Siku mbili zilizopita, wapiganaji wengi walitumia njia hiyo. Kwa jumla, wanamgambo 2,000 na familia zao wataondoka kutoka kusini mwa jimbo la Damascus.

Lakini hata kabla ya kumalizika kwa zoezi hili, raia 5000 wazaliwa wa eneo hili wamerejea katika eneo la Qadam jirani na maeneo mengine jirani. Walikua wakiishi, kwa kipindi cha miaka mitatu, katika makambi ya nyumba za kuhamishwa, ziliowekwa na serikali nje kidogo magharibi mwa mji wa Damascus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.