Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-HIJA-CORONA-AFYA

Saudia yaruhusu ibada ya Hija lakini marufuku kwa wageni

Saudi Arabia imetangaza kwamba ibada takatifu ya Hija itafanyika mwishoni mwa mwezi wa Julai, lakini kwa raia waishio nchini humo pekee. Kumekuwa na hofu kwamba Hija inaweza kufutwa kabisa.

Kwa kawaida Hija ni moja ya ibada muhimu Waislamu, na ni mojawapo ya nguzo tano za Kiislamu ambayo kila Muislamu hutakiwa kuitekeleza walau mara moja kwa uhai wake kama ana uwezo wa kifedha na kiafya.
Kwa kawaida Hija ni moja ya ibada muhimu Waislamu, na ni mojawapo ya nguzo tano za Kiislamu ambayo kila Muislamu hutakiwa kuitekeleza walau mara moja kwa uhai wake kama ana uwezo wa kifedha na kiafya. AHMAD AL-RUBAYE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuja wakati huu nchi hiyo ikiendele kukabiliana na janga hatari la Covid-19.

Saudi Arabia imerekodi visa laki 161,000 vya maambukizi ya Corona baada ya visa vipya 3,393 kuthibitishwa , na watu 1,307 wamefariki dunia, baada ya vifo vipya 40 kuthibitishwa kulingana na kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, huku wagonjwa zaidi ya laki moja wakipona ugonjwa huo hatari.

Kwa kawaida Hija ni moja ya ibada muhimu Waislamu, na ni mojawapo ya nguzo tano za Kiislamu ambayo kila Muislamu hutakiwa kuitekeleza walau mara moja kwa uhai wake kama ana uwezo wa kifedha.

Raia kutoka nchi nyingine ambao tayari ni wakazi wa Saudi Arabia ndio wataruhusiwa kuhudhuria Hija ya mwaka huu pamoja na raia wa nchi hiyo ambao wanaishi nchini humo.

Maafisa nchini humo wanasema hii ndio njia pekee itakayowezesha kufanya mipango ya kutokaribiana ambayo itawezesha watu wawe salama.

Hii itakuwa mara ya kwanza Saudia inalazimika kuchukua tahadhari kama hiyo ya kuwazuia waislamu kufanya ziara hiyo ambayo ni mojawapo ya nguzo ya dini ya Kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.