Pata taarifa kuu

Watu kadhaa watekwa nyara katika kituo cha polisi nchini Pakistani

Vikosi maalum vya Pakistan vimemaliza vitendo vya utekaji nyara vilivyofanywa na wanamgamo wa Taliban nchini Pakistani katika kituo cha polisi huko Bannu kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, na kuripoti vifo lakini bila kutaja idadi.

Wanajeshi wakiwasili na kuchukua nafasi karibu na eneo la kituo cha polisi baada ya kushambuliwa huko Bannu Februari 14, 2013. Wanamgambo sita wanaoaminika kuwa washambuliaji wa kujitoa mhanga waliuawa na polisi mmoja alijeruhiwa wakati polisi wakikabiliana na mashambulizi makubwa ya wanamgambo kwenye kituo cha polisi cha Maryan katika Mkoa wa Frontier Bannu siku ya Alhamisi, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Wanajeshi wakiwasili na kuchukua nafasi karibu na eneo la kituo cha polisi baada ya kushambuliwa huko Bannu Februari 14, 2013. Wanamgambo sita wanaoaminika kuwa washambuliaji wa kujitoa mhanga waliuawa na polisi mmoja alijeruhiwa wakati polisi wakikabiliana na mashambulizi makubwa ya wanamgambo kwenye kituo cha polisi cha Maryan katika Mkoa wa Frontier Bannu siku ya Alhamisi, vyombo vya habari vya ndani viliripoti. REUTERS/Zahid Mohammad
Matangazo ya kibiashara

"Operesheni hiyo ilikamilika kwa mafanikio," Waziri wa Ulinzi Khawaja Muhammad Asif amesema katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Islamabad, na kuongeza kuwa baadhi ya mateka "wamepoteza maisha."

Siku ya Jumapili, zaidi ya wanachama 30 wa kundi la Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), waliokamatwa kwa tuhuma za ugaidi, walikamata silaha kutoka kwa maafisa waliokuwa wakiwahoji katika kituo cha polisi cha Bannu katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, kaskazini-magharibi mwa Pakistan.

Waziri huyo amebainisha Jumanne kwamba vikosi maalum viliingilia kati wakati tofauti zilipozuka kati ya wanaodaiwa kuwa wapignaji wa TTP kuhusu jinsi ya kuwashughulikia mateka hao.

Watekaji nyara walitaka kupita salama hadi Afghanistan ili waweze kuwaachiliwa huru mateka, angalau maafisa wanane wa polisi na maafisa wa ujasusi wa kijeshi, Muhammad Ali Saif, msemaji wa serikali ya mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, amesema.

Shule, pamoja na ofisi na barabara zimefungwa Jumanne katika eneo hilo na vituo vya ukaguzi viliwekwa katika eneo jirani. TTP imedai kuwajibika kwa kuchukua mateka katika eneo hili lililo kwenye mpaka na Afghanistan ambako lina mizizi imara zaidi.

TTP, tofauti na Taliban ya Afghanistan lakini ikiongozwa na itikadi sawa, ilimaliza usitishaji wa mapigano na Islamabad mnamo Novemba 28 na kuahidi kufanya mashambulio kote Pakistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.