Pata taarifa kuu

Mkutano wa UN kuhusu Afghanistan umeanza nchini Qatar

Nairobi – Mkutano wa siku mbili wa umoja wa Mataifa kuhusu nchi ya Afghanistan, umeanza rasmi mjini Doha, Qatar, licha ya kutokuwepo kwa ujumbe wa Taliban.

Washiriki watajadiliana namna ya kushirikiana na Taliban
Washiriki watajadiliana namna ya kushirikiana na Taliban © Abdul Khaliq / AP
Matangazo ya kibiashara

Washiriki watajadiliana namna ya kushirikiana na Taliban katika utaratibu unaofaa chini ya tathmini huru iliyoazimiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwaka jana.

Hata hivyo haijafahamika ikiwa viongozi wa Taliban watashirikia baadae kongamano hilo, ingawa umoja wa Mataifa unasema ulituma mwaliko kwa utawala Kabul, ambao unadai ulitoa masharti kadhaa ili kushiriki mazungumzo hayo.

Mkutano huu mahsusi uliitishwa na katibu mkuu wa UN Antonio Guterres, ambapo aliwaalika wajumbe kutoka nchi 25, zikiwemo asasi za kiraia, makundi ya wanawake, Uchina na umoja wa Ulaya.

Tangu Taliban irejee madarakani mwaka 2021, kumekuwa na shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa kwa utawala huo kuhuisha makundi yote kwenye Serikali ikiwemo wanawake ambao wametupwa nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.