Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Harambee Stars kukipiga na Lesotho katika Michuano ya Kombe la COSAFA

Timu ya taifa ya soka ya Kenya inashuka dimbani leo hii kumenyana na Lesotho katika mchezo wake kwa kwanza kutafuta ubingwa wa taji la COSAFA.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars
Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo unachezwa katika uwanja wa Arthur Davies jijini Kitwe nchini Zambia na licha ya kulenga kutwaa taji hilo la Mataifa ya Kusini mwa Afrika, Harambee Stars inatumia mechi hizi kujiandaa kwa mchuano wa mwisho wakufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao dhidi ya Nambia mwezi Septemba.
 

Kenya ilialikwa katika mashindano hayo na itamenyana na Swaziland katika mchuano wake wa pili siku ya Jumanne na baadaye Bostwana siku ya Alhamisi .
 

Hata hivyo kikosi cha Harambee Stars chini ya kocha Adel Amrouche kinawajumuisha wachezaji wanaocheza soka katika ligi ya nyumbani baada ya wachezaji wanaosakata soka la kulipwa kushindwa kujiunga na kikosi hicho.
 

Mshindi wa kundi hilo atakutana na Angola katika mchezo wa robo fainali baadaye mwezi huu.
 

Namibia walianza vema kampeni zao kwa kuwashinda Mauritius kwa mabao 2 kwa 1 mwishoni mwa juma lililopita na ikiwa watawashinda Ushelisheli Jumatatu hii watafuzu katika hatua ya robo fainali na kumenyana na Afrika Kusini.
 

Swaziland walitoka sare ya kutofungana na Bostwana.
 

Mtaifa mengiene ambayo yamefuzu katika robo fainali ni pamoja na mabingwa watetezi Zimbabwe, na wenyeji wa mashindano haya Zambia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.