Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA WINGEREZA

Southampton yaburuzwa kwa mabao 3-0

Manchester City imepanda nafasi ya pili baada ya kuiburuza Southampton Jumapili novemba 30 kwa mabao 3-0. Machester city ina pointi sita nyuma ya Chelsea.

Manchester City yapanda nafasi ya pili baada ya kuifunga southampton mabao 3-0, Jumapili Novemba 30 mwaka 2014.
Manchester City yapanda nafasi ya pili baada ya kuifunga southampton mabao 3-0, Jumapili Novemba 30 mwaka 2014. REUTERS/Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, Manchester City ilifaulu kuishinda Bayern kwa mabao 3-2, baada ya Agüero kuweka wavuni bao la ushindi. Yaya Touré hakucheza mchuano huo. Hata hivyo Manchester City ilifanya vizuri ikiwa nyumbani na kufuzu katika mzunguko wa nane wa ligi ya mabingwa.

Machester City ilianza vibaya katika mchuano huo, kufuatia kukosekana uwanjani kwa Yaya Touré, ambaye aliondolewa uwanjani katika mechi iliyotangulia baada ya kupewa kadi nyekundu.

Licha ya kuwa idadi ya wachezaji ilikua imepungua, Bayen ilikuja juu na kusawazisha katika dakika ya 40. Bao hilo lilwekwa kimyani na Xabi Alonso. Baada ya dakika 5, Bayern iliingiza bao la pili, na kuongoza ikiwa na mabao 2-1.

Hadi mwisho wa kipindi cha kwanza cha mchezo, Bayern ilikua ikiongoza kwa mabao 2-1. Lakini hali ya mchezo ilibadilika, wakati ambapo Bayern ilikosa mabao mengi, huku  Xabi Alonso, akipoteza mpira, na kuchukuliwa na Agüero, ambaye alifaulu kuingiza bao la pili na kupelekea klabu yake ya Manchester City kuwa sare ya mabao 2-2 na Bayern. Bao hilo la kusawazisha liliingizwa wavuni katika dakika ya 85.

Agüero alifaulu katika dakika ya 90 kuingiza bao la ushindi, na kupelekea Manchester City kuishinda bayern mabao 3-2.

Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema kikosi chake ni imara kuweza kukabiliana na Chelsea katika mbio za kuusaka ubingwa wa ligi ya Uingereza baada ya kuibwagiza Southamton mabao 3-0.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.