Pata taarifa kuu
TANZANIA-CAF-SOKA-

Mkwasa ataja kikosi cha Taifa Stars kumenyana na Uganda

Kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars, amekitaja kikosi cha wachezaji 26 wanaocheza soka nchini humo kwa maandalizi ya mchuano wa marudiano dhidi ya Uganda kufuzu katika fainali za michuano ya CHAN mapema mwezi ujao jijini Kampala.

Dutchman Mart Nooij, kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ( Taifa Stars).
Dutchman Mart Nooij, kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ( Taifa Stars).
Matangazo ya kibiashara

Mkwasa amesema yeye pamoja na msaidizi wake Hemed Morocco wameteua kikosi cha wachezaji wanaoamini wanaweza kuleta mabadiliko katika timu ya taifa baada ya matokeo mabaya katika michuano iliyopita.

Kikosi hiki kinatarajiwa kuanza mazoezi siku ya Ijumaa wiki hii nje ya jiji la Dar es Salaam tayari kupambana na Uganda na kujiandaa katika michuano ya kufuzu katika fainali za AFCON mwaka 2017 nchini Gabon.

Kocha huyo mpya amesema lengo lao ni kuinua kiwango cha soka nchini Tanzania na kuleta mabadiliko katika timu ya taifa.

“ Tunaahidi kuwa angalau tutaleta mabadiliko katika kikosi cha taifa Stars, tunatambua kuwa haitakuwa rahisi ila tunaamini kuwa kikosi hiki kitaleta mabadiliko”, amesisitiza Mkwasa.

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limempa kibarua hicho baada ya kuachishwa kazi kwa Mholanzi Mart Nooij kutokana na matokeo mabaya katika michuano ya kimataifa.

Kikosi kamili:

Makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ali (Azam FC) na Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga).

Mabeki: Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Aggrey Morris (Azam FC).

Viungo wa kati: Jonas Mkude (Simba SC), Abdi Banda (Simba SC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Simba SC) na Deus Kaseke (Mbeya City).

Washambuliaji: Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Ame Ali (Mtibwa Sugar), wakati wengine ambao wamewekwa akiba ni Juma Abdul wa (Yanga SC), Mudathir Yahya wa (Azam FC) na Samuel Kamuntu wa (JKT Ruvu).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.