Pata taarifa kuu
AFRIKA-KOMBE LADUNIA 2018-SOKA

Timu sita zaingia katika hatua ya makundi

Timu za taifa sita ikiwani pamoja na Uganda, Guinea, Gabon, Zambia, Jamhuri ya Kidemmokrasia ya Congo na Morocco zimeingia katika hatua ya makundi ya kutafuta tiketi ya Kombe la Dunia 2018 nchi Urusi.

Wajezaji wa timu ya taifa ya Morocco kila mmoja akimpongeza mwengine wakati wa ushindi dhidi ya Libya, katika michuano ya mchujo Chan 2016.
Wajezaji wa timu ya taifa ya Morocco kila mmoja akimpongeza mwengine wakati wa ushindi dhidi ya Libya, katika michuano ya mchujo Chan 2016. AFP PHOTO / FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kupata ushindi ugenini siku tatu zilizopia timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitoka sare ya mabo 2-2 na Burundi katika uwanja wa Martyr jijini Kinshasa, na hivyo kupelekea Leopard kuingia katika hatua ya makundi baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 huko Bujumbura.

Uganda, wakicheza nyumbani katika uwanja wa Mandela waliifunga Togo 3-0. Katika mechi ya walai nchini Togo, Uganda iliifunga Togo bao moja kwa nunge. Kufuatia ushindi wa Jumpili hii jijini Kampala timu ya taifa ya Uganda imeshinda kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Togo.

Gabon wameingia katika hatua ya makundi kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Msumbiji.

Zambia, imeiburuza Sudan kwa mabao 2-0. Mchuano wa awali Zambia iliifunga Sudan bao 1-0, na hivyo Zambia kufuzu kwa makundi kwa jumla ya mabao 3-0. Mabao ya Zambia Jumapili hii yalifungwa na Lubambo Musonda na Winston Kalengo.

Kwa upande wake Morocco wamefungwa na Equatorial Guinea bao moja kwa nunge. Morocco licha ya kufungwa katika mchuano wa Jumapili hii, imeingia katika hatua ya makundi kufuatia ushindi walioupata katika mechi ya awali ambapo iliifunga Equatorial Guinea mabao 2-0.

Timu hizi za Uganda, Guinea, Gabon, Zambia, Jamhuri ya Kidemmokrasia ya Congo na Morocco zitaungana na timu nyingine 14 zitakazofuzu Jumanne na kupangiwa makundi matano ya timu 4 kila kundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.