Pata taarifa kuu
AFRIKA-KOMBE LADUNIA 2018-SOKA

Kombe la Dunia 2018: timu kutoka Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati zaondolewa

Timu ishirini za Afrika ambazo zimeingia katika hatua ya makundi ya kufuzu kwa Kombe la soka duniani 2018 zimejulikana. Burkina Faso, Cameroon, Congo, Côte d’Ivoire, Mali na Senegal zimepata ushindi Jumanne Novemba 17 katika duru ya pili ya michuano ya kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la soka la Dunia 2018.

Wachezaji wa Côte d’Ivoire wakifurahia ushindi wao dhidi ya Liberia katika mchuano wa kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la soka la Dunia 2018.Coupe du monde 2018.
Wachezaji wa Côte d’Ivoire wakifurahia ushindi wao dhidi ya Liberia katika mchuano wa kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la soka la Dunia 2018.Coupe du monde 2018. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande mwengine, Tanzania, Kenya, Rwanda , Ethiopia zote kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zimeondolewa katika kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kufuzu katika kombe la dunia katika mchezo wa soka, michuano itakayofanyika nchini Urusi mwaka 2018.

Taifa Stars ya Tanzania ikicheza ugenini jijini Algers ilifungwa na wenyeji wao mabao 7 kwa 0, matokeo ambayo yamewahuzunisha mashabiki wa soka nchini humo ambao wlaikuwa wanatazama mchezo huo jana usiku.

Harambee Stars ya Kenya ambayo ilikuwa na matataizo mengi ya wachezaji kutolipwa marupurupu, kuchelewa kuondoka Naiorobi baada ya kusuburi kwa saa nane walifungwa na Cape Verde mabao 2 kwa 0.

Rwanda nayo ikiwa nyumbani jijini Kigakli ilipoteza kwa kufungwa mabao 3 kwa 1 na Libya, huku Congo Brazaville ikiifunga Ethiopia mabao 2 kwa 1.

Ni Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zilizofanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi kutoka eneo la Afrika Mashariki na Kati kujaribu kutafuta mataifa matano yatakafuzu kwenda kushirki katika mashindano hayo.

Kombe la Dunia 2018: Matokeo ya michuano mbalimbali barani AFRIKA *

*Kwa herufi nene, ni timu zilizopata ushindi

Gabon – Msumbiji 1-0, 4-3 tab, jijini Libreville
Uganda – Togo 3-0, jijini Kampala
Zambia – Sudan 2-0, jijini Ndola
DRCongo – Burundi 2-2, jijini Kinshasa
Equatorial Guinea – Morocco 1-0, jijini Bata
Guinea – Namibia 2-0, jijini Casablanca (Morocco)
Rwanda – Libya 1-3, à Kigali
 

Cameroon – Niger 0-0, jijini Yaoundé
Congo – Ethiopia 2-1, jijini Brazzaville
Nigeria – Swaziland 2-0, jijini Port Harcourt
Ghana – Comoros 2-0, jijini Kumasi
Misri – Chad 4-0, jijini Cairo
Tunisia – Mauritania 2-1, jijini Radès
Afrika Kusini – Angola 1-0, jijini Durban
Côte d’Ivoire – Libéria 3-0, jijini Abidjan
Burkina Faso – Benin 2-0, jijini Ouagadougou
Algeria – Tanzania 7-0, jijini Blida
Cape Verde – Kenya 2-0, jiji Praia
Senegal – Madagascar 3-0, jijini Dakar
Mali – Botswana 2-0, jijini Bamako
 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.