Pata taarifa kuu
KENYA-WADA-RIADHA

WADA yaipa Kenya siku 26

Shirika la Kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa wanariadha (Wada) limeiongezea Kenya muda wa karibu mwezi mmoja hadi Mei 2 ili ihakiki sheria mpya za kumpamaba na kusambaa kwa matumizi ya madawa haramu katika Riadha.

Thomas Longosiwa, mmoja wa wanariadha wa Kenya.
Thomas Longosiwa, mmoja wa wanariadha wa Kenya. AFP PHOTO/MONIRUL BHUIYAN
Matangazo ya kibiashara

Awali Kenya ilipewa makataa ya hadi mwezi Februati lakini ikashindwa kutekeleza.

Kenya ilipewa onyo la kupitisha sheria hiyo mpya la sivyo ipigwe marufuku ya kutoshiriki mashindano ya kimataifa baada ya kuenea kwa matumizi ya madawa hayo yaliyopigwa marufuku miongoni mwa wanariadha wake.

Jumatao hii Kamati ya kutekeleza kanuni za Wada ilikutana nchini Canada na kuafikiana kuipa Kenya makataa ya kuhakikisha kuwa chama kipya kinachopambana na matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku nchini Kenya NADO na taasisi ya kupambana na madawa hayo haramu ADAK zinapewa msingi wa kisheria unaoendana na sheria za WADA.

Itafahamika kwamba licha ya kuwa Kenya ni mabingwa wa dunia katika Riadha, mpaka sasa wanariadha wake 40 wamepatikana na hatia ya kutumia madawa ya kusisimua muili yaliopigwa marufuku.

Kamati kuu ya WADA itakutana tena tarehe 12 mwezi Mei Montreal nchni Canada kujadili hatua ambazo Kenya itakuwa imetekeleza kuhakikisha sheria hiyo mpya imepewa msingi wa kikatiba.

Katiba ya Kenya inaamuru mswada ufikishwe bungeni mara mbili na kujadiliwa mara mbili ili upigwe msasa kikamilifu kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria.

Hadi kufikia tarehe hiyo iwapo Kenya itakuwa haijaidhinisha sheria hiyo itachukuliwa kama nchi ambazo zinahujumu vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kusisimua mwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.