Pata taarifa kuu
KENYA-RIADHA-IAAF

Kenya kupambana na dawa zilizopigwa marufuku na WADA

Hatimaye Kenya, imepata sheria ya kupambana na wanamichezo wanaotumia dawa za kusisimua misuli, sharti lililokuwa imewekewa na Shirika la Kimatifa la kupambana na dawa hizo WADA na Shirikisho la riadha duniani IAAF.

Wanariadha Kenya wakishiriki mashindano, mwaka 2011.
Wanariadha Kenya wakishiriki mashindano, mwaka 2011. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kenya ilikuwa imepewa hadi tarehe 2 mwezi ujao kuwa na sheria hiyo au la ifungiwe kushiriki katika mashindano ya Olimpiki mwezi Agosti mwaka huu nchini Brazil.

Rais Kenyatta ametia saini sheria hiyo katika Ikulu ya Nairobi hivi leo, hatua ambayo imewafurahisha sana wanamichezo hasa wanaraidha nchini humo.

Kenyatta ameongeza kuwa hakutakuwa na sababu yoyote ya Kenya kutoshriki mashindano ya Olimpiki na kufanya vizuri duniani.

Kwa mujibu wa sheria hii, mwanamichezo yeyote atakayebainika kutumia dawa zilizopigwa marufuku atatozwa faini ya Dola elfu moja au kufungwa ajela mwaka mmoja, na wale watakaopatikana kuingiza dawa hizo nchini Kenya au daktari atakayepatikana na dawa hizo akimpa mwanamichzo atatozwa faini ya Dola elfu 30 au kufungwa jela miaka mitatu.

Maafisa wa Shirika la WADA watakutana tarehe 12 mwezi ujao mjini Montreal nchini Canada kupigia kura sheria hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.