Pata taarifa kuu
WADA

Wadukuzi kutoka Urusi watoa taarifa zaidi za wanamichezo walizoiba

Wadukuzi wa mitandaoni wanaodaiwa kutoka Urusi, wametoa taarifa zaidi ya kiafya za wachezaji mbalimbali walizoiba kutoka Shirika la dunia linalopiga vita matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa wanamichezo (Wada).

Jengo la Shirika la WADA linalopambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo duniani
Jengo la Shirika la WADA linalopambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo duniani REUTERS/Christinne Muschi
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zilizotolewa ni za mkimbiza Baiskeli kutoka nchini Uingereza Bradley Wiggins, aliyeshinda medali ya dhahabu katika Michezo iliyokamilika ya Olimpiki nchini Brazil mwezi Agosti mwaka huu.

Bingwa mara tatu wa mashindano ya Tour de France nchini Ufaransa Chris Froome, taarifa zake za kiafya pia zimewekwa wazi.

Hata hivyo, imebainika kuwa wachezaji hao hawakutumia dawa zozote za kuwaongezea nguvu mwilini kuwasaidia kupata ushindi.

Shirika la WADA linasema wizi wa taarifa hizo uliofanywa na wadukuzi hao kutoka Urusi, unalenga kuingilia na kulichafulia jina kutokana na harakati zake za kuhakikisha kuwa wanamichezo duniani hawatumii dawa zilizopigwa marufuku.

Wadukuzi hao wanaofahamika kama "Fancy Bears" wamesema wameamua kuiba taarifa hizo na kuziweka wazi kwa kile wanachodai kuwa viongozi wa WADA ni waongo na wafisadi.

Mapema wiki hii, wadukuzi hawa pia walitoa ripoti za kiafya za wachezaji wa Tennis kutoka Marekani Serena William, na wanamichezo wengine kutoka Uingereza na Ujerumani.

WADA imekuwa ikiwashuku wanamichezo wa Urusi kwa kutumia dawa za kuwaongezea nguvu mwilini, na wanamichezo wake walizuiliwa kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya walemavu inayoendelea nchini Brazil.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.