Pata taarifa kuu
SOKA-EURO 2020

Uingereza yafuzu kucheza fainali ya Euro

Uingereza imefuzu fainali ya kuwania kombe la soka barani Ulaya, baada ya kuifunga Denmark mabao 2-1 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa jana usiku katika uwanja wa Wembley jijini London.

Timu ya taifa ya Uingereza ikisherehekea baada ya kufuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la Euro Julai 07 2021
Timu ya taifa ya Uingereza ikisherehekea baada ya kufuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la Euro Julai 07 2021 Laurence Griffiths POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Denmark ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika 30 kupitia mchezaji wake Mikkel Damsgaard, lakini Uingereza ikasawazisha dakika tisa baadaye baada ya Denmark kujifunga kupitia mchezaji wake Simon Kjaer.

Mpaka dakika 90, timu zote zilikuwa sare kwa bao moja kwa muda na kulazimu mechi hiyo kwenda mpaka muda wa ziada na ilipofika dakika ya 104, Harry Kane alikuwa shujaa wa timu yake baada ya kupachika bao la pili na la ushindi.

Uingereza sasa itamenyana na Italia katika ya fainali siku ya Jumapili. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.