Pata taarifa kuu

Michael Wokorach, Mchezaji wa Raga nchini Uganda amestaafu

NAIROBI – Nahodha wa timu ya Uganda ya Raga ya Wachezaji saba kila Upande na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Rugby Cranes, Michael Wokorach ametangaza kustaafu kucheza raga ya kimataifa.

Nahodha wa timu ya Uganda ya Raga ya Wachezaji saba kila Upande na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Rugby Cranes, Michael Wokorach ametangaza kustaafu kucheza raga ya kimataifa.
Nahodha wa timu ya Uganda ya Raga ya Wachezaji saba kila Upande na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Rugby Cranes, Michael Wokorach ametangaza kustaafu kucheza raga ya kimataifa. © Michael Wokorach
Matangazo ya kibiashara

Mei Mosi ikiwa ni siku ya Leba Dei ambayo huwa ni sherehe kwa wafanyikazi, Wakoraha aliamua kutumia mtandao wa twitter kutangaza taarifa hizo kwa raia wa Uganda na mashabiki wake.

Wakorach pia alimpongeza nahodha mpya Ian Munyani, ambaye alimkabidhi rasmi majukumu ya unahodha mwishoni mwa juma wakati wa mashindano ya dunia ya raga ya Sevens Challenger Series 2023. Munyani atasaidiwa na Aaron Ofoyrwoth kufuatia kuondoka kwa Wokorach.

Wokorach alikuwa na taaluma yenye mafanikio katika uongozi wake kwenye timu ya taifa ya raga Uganda aliyoongoza kwa muda wa zaidi ya Muongo mmoja.

Alicheza na kuwa nahodha wa Uganda katika hafla nne za michezo ya jumuiya ya madola tangu 2010, hafla tano za Challenger Series tangu 2020, hafla mbili za kombe la dunia la rugby sevens tangu 2018, Rugby Africa Men's Sevens tangu 2010, na hafla nyingi za Mzunguko wa Dunia wa Raga Sevens World Series.

Hata hivyo, anaondoka Uganda Men's Sevens akiwa na biashara ambayo haijakamilika ya kufuzu kwa HSBC World Rugby Sevens Series. Ni ndoto yake, pamoja na kwenda kwenye Michezo ya Olimpiki.

Sio mara ya Kwanza kwa Warokah Kustaafu kwani Mnamo 2019, alistaafu kuichezea timu ya Taifa  Rugby Cranes lakini alitangaza kupatikana kwake miaka miwili baadaye kufuatia kifo cha mkufunzi wake mpendwa Robert Seguya.

Wakongwe wengine wa raga walioacha raga na kutangaza kupatikana kwao tena nchini Uganda ni pamoja na Wachezaji Dennis Etuket , Allan Musoke na Kocha wa zamani Timothy Mudoola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.