Pata taarifa kuu

Haaland ndiye mchezaji bora wa ligi kuu na anayechipukia

NAIROBI – Erling Haaland wa Manchester City amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza na lile la mchezaji mchanga kwa msimu mmoja.

Erling Haaland wa Manchester City anasherehekea taji la Ligi Kuu ya England baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Manchester City na Chelsea kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, Uingereza, Jumapili, Mei 21, 2023. (AP Photo/Jon Super)
Erling Haaland wa Manchester City anasherehekea taji la Ligi Kuu ya England baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Manchester City na Chelsea kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, Uingereza, Jumapili, Mei 21, 2023. (AP Photo/Jon Super) AP - Jon Super
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amecheza mechi 35 pekee na kuweka rekodi mpya ya ligi Kuu ya Uingereza ya kufunga mabao 36 ndani ya msimu mmoja na kuisaidia Manchester City kuhifadhi taji hilo.

"Nimenyenyekea kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo zote mbili kwa msimu mmoja - asante kwa kila mtu aliyenipigia kura," Haaland alisema katika taarifa ya City.

"Umekuwa msimu wa kwanza wa ajabu katika ligi kuu na kushinda  kombe wikendi iliyopita mbele ya mashabiki wetu pale Etihad ilikuwa wakati wa kipekee sana kwangu."

Erling Haaland wa Manchester City
Erling Haaland wa Manchester City © Manchester City

Raia huyo wa Norway, ambaye pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa waandishi wa kandanda wiki hii, amefunga mabao 52 katika michuano yote huku City ikikaribia kushinda mataji matatu.

Vijana wa Pep Guardiola watamenyana na Manchester United katika fainali ya Kombe la FA na Inter Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwezi ujao.

 "Tuzo hizi zisingewezekana bila wachezaji wenzangu, meneja na wafanyikazi wote kwenye klabu ambao hunisaidia kufanya vizuri uwanjani," aliongeza Haaland.

 "Sasa tuna fainali mbili zaidi na tunataka kumaliza msimu tukiwa na nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.