Pata taarifa kuu

Anthony Taylor: PGMOL imekashifu unyanyasaji unaoelekezwa dhidi ya mwamuzi huyo

NAIROBI – Bodi ya waamuzi PGMOL inasema inashangazwa na unyanyasaji "usio na msingi na wa kuchukiza" ulioelekezwa kwa Anthony Taylor katika uwanja wa ndege wa Budapest baada ya fainali ya ligi ya Europa siku ya Jumatano Jumatano.

PGMOL  inalaani unyanyasaji unaoelekezwa dhidi ya mwamuzi Anthony Taylor
PGMOL inalaani unyanyasaji unaoelekezwa dhidi ya mwamuzi Anthony Taylor REUTERS - JOHN SIBLEY
Matangazo ya kibiashara

Muingereza huyo ndiye alikuwa mwamuzi wa mchezo huo, ambapo Sevilla waliwafunga Roma kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1.

Taylor na familia yake  walizomewa na mashabiki wenye hasira kwenye uwanja wa ndege baada ya mechi hiyo.

Kabala ya mashabiki kumzomea mwamuzi huyo, awali kocha wa Roma Jose Mourinho alionekana kwenye sehemu ya maegesho ya magari akimkabili mwamuzi huyo kwa maneno makali na machafu.

Kocha  AS Roma  Jose Mourinho alieleza kukasirishwa na maamuzi ya Antony Tylor, REUTERS/Annegret Hilse
Kocha AS Roma Jose Mourinho alieleza kukasirishwa na maamuzi ya Antony Tylor, REUTERS/Annegret Hilse REUTERS - ANNEGRET HILSE

PGMOL  katika taarifa yake imesema kuwa inafahamu kuhusu video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Anthony Taylor na familia yake wakinyanyaswa  katika uwanja wa ndege wa Budapest.

"Tumeshtushwa na unyanyasaji usio na msingi na wa kuchukiza unaoelekezwa kwa Anthony na familia yake anapojaribu kurejea nyumbani baada ya fainali ya Uefa Europa League.

"Tutaendelea kutoa msaada wetu kamili kwa Anthony na familia yake."

Wakati huo huo, Uefa inasubiri ripoti kutoka kwa maafisa wa mechi na wajumbe kabla ya kuamua kuchukua hatua dhidi ya Mourinho kuhusiana na tukio tofauti katika maegesho ya magari baada ya mechi.

Mwamuzi Anthony Taylor, wakati wa mechi kati ya Roma dhidi ya Sevilla, Jumatano, Mei 31, 2023. (AP Photo/Darko Bandic)
Mwamuzi Anthony Taylor, wakati wa mechi kati ya Roma dhidi ya Sevilla, Jumatano, Mei 31, 2023. (AP Photo/Darko Bandic) AP - Darko Bandic

Mourinho alimkosoa Taylor katika mkutano wake na wanahabari na baadaye alinaswa akifoka na kutoa maoni ya wazi wakati Taylor na maafisa walikuwa wakiabiri  basi dogo.

Taylor alitoa kadi za njano kwa wachezaji 13, idadi ya juu zaidi kwenye mchezo wa Ligi ya Europa. Saba kati yao walikuwa wachezaji wa Roma, rekodi ya fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.