Pata taarifa kuu

Man City na Inter Milan wanajiandaa kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa

NAIROBI – Manchester City na Inter Milan wanapambana katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi mjini Istanbul huku timu ya Uingereza, chini ya Pep Guardiola, ikiwa na matarajio makubwa  ya kushinda taji kubwa zaidi ya vilabu vya Ulaya kwa mara ya kwanza.

Manchester City wanacheza dhidi ya Inter Milan kuwania klabu bingwa barani Ulaya. REUTERS/Mehmet Emin Caliskan
Manchester City wanacheza dhidi ya Inter Milan kuwania klabu bingwa barani Ulaya. REUTERS/Mehmet Emin Caliskan REUTERS - EMIN CALISKAN
Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itacheza  katika Uwanja wa Olimpiki wa Ataturk wenye viti 75,000, itaanza saa nne  usiku kwa saa za Afrika Mashariki  katika jiji kuu la Uturuki.

Guardiola amejenga kikosi ambacho kinadaiwa kucheza soka bora kuliko timu yoyote tangu alipoinoa klabu ya Barcelona ya muongo mmoja uliopita, huku akifukuzia taji la tatu la Ligi ya Mabingwa katika maisha yake ya ukocha.

Iwapo atashinda taji hili, atakuwa kocha wa nne kushinda kombe hilo zaidi ya mara mbili.

 "Ni ndoto kabisa," Mhispania huyo alisema Ijumaa.

Hiyo ni fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa kwa City katika misimu mitatu, miaka miwili baada ya kushindwa na Chelsea mjini Porto, na wanatumai kushinda mataji matatu baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA.

Timu ya mwisho ya Uingereza kushinda mataji matatu kwa msimu mmoja ilikuwa Manchester United ya Alex Ferguson, mnamo 1999.

"Tumekuwa wazuri katika mashindano haya, lakini tunahitaji kutafuta njia ya kushinda taji  la kwanza," alisema Kevin De Bruyne.

Kevin de Bruyne (Manchester City)
Kevin de Bruyne (Manchester City) © Dave Thompson/AP

"Ikiwa tutafanya hivyo, ni wazi litakuwa jambo kubwa kwa wachezaji, kwa klabu, na kwa mashabiki litakuwa jambo la kushangaza."

Mafanikio ya City yamewezeshwa na uwekezaji kutoka Kundi la Abu Dhabi United, ambao ulipelekea wao kupata mapato makubwa zaidi katika kandanda ya dunia mwaka 2022 ya euro milioni 731 ($787m).

Mechi ya leo ya klabu bingwa kati ya Manchester City dhidi ya Inter Milan inachezwa mjini Instanbul
Mechi ya leo ya klabu bingwa kati ya Manchester City dhidi ya Inter Milan inachezwa mjini Instanbul REUTERS - UMIT BEKTAS

City wameonyesha mchezo bora katika mashindano haya baada ya  kuwaondoa RB Leipzig, Bayern Munich na Real Madrid katika raundi ya mtoano na wamepoteza mara moja tu katika mechi 27.

Erling Haaland amefunga magoli  52 katika mashindano yote, mabao amabao yamewasaidia City kupanda hadi kiwango kingine, pamoja na uamuzi wa Guardiola kumgeuza beki wa kati John Stones kuwa kiungo.

Erling Haaland amekuwa mwenye manufaa zaidi kwa klabu ya Manchester City
Erling Haaland amekuwa mwenye manufaa zaidi kwa klabu ya Manchester City REUTERS - MOLLY DARLINGTON

Pande zote mbili zinapaswa kuwa na nguvu ya kutosha kuelekea mechi ya leo , huku Kyle Walker akitarajiwa kuanza kuichezea City baada ya kukosa mazoezi mapema wiki hii.

Hii ni fainali ya sita ya kombe la Ulaya kwa Inter, lakini ni fainali yao ya pili ndani ya miaka 51.

Taji pekee la Uropa la City kufikia sasa ni 1970, walipotwaa Kombe la Washindi, kwa kuwalaza Gornik Zabrze ya Poland 2-1 kwenye fainali.

Iwapo wataishinda Inter, litakuwa jina jipya la kwanza kwenye kombe hilo tangu Chelsea mwaka 2012.

Wachezaji wa Inter Milan
Wachezaji wa Inter Milan AFP - GABRIEL BOUYS

Pia itamaanisha Manchester ni jiji la pili kutoa washindi wawili tofauti wa shindano hilo, baada ya Milan.

Ni fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa iliyofanyika katika Uwanja wa Olimpiki wa Ataturk, ulioko upande wa Ulaya wa Bosphorus, kilomita 25 kutoka katikati mwa Istanbul.

Liverpool ilishinda hapa mwaka wa 2005, ikipata ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Milan na kutoka sare ya 3-3 kabla ya kushinda kwa mikwaju ya penalti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.