Pata taarifa kuu
AFCON 2027

Ramani ya Afcon 2027 yazinduliwa

Diani, Kenya – Kenya, Uganda na Tanzania zimetoa ramani rasmi ya kuandaa Kombe la Mataifa bingwa barani Afrika ya mwaka 2027. 

MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI KENYA, FKF BARRY OTIENO 1
MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI KENYA, FKF BARRY OTIENO 1 © rfi Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Katika ramani hiyo iliyowasilishwa na mkurugenzi mkuu wa shirikisho la soka nchini Kenya, Barry Otieno – viwanja vyote vinafaa viwe tayari kufikia tarehe 31 Disemba 2025, jopo la kusimamia mashindano kubuniwa pamoja na bajeti yake kutolewa kufikia Agosti 2027.  

Kamati ya mashindano itaundwa kuanzia Februari tarehe moja hadi Machi 24 2024, mauzo na kutangaza mashindano hayo yataanza mara moja hadi Agosti 27, 2027.

Kikao cha washikadau kwenye majadiliano
Kikao cha washikadau kwenye majadiliano © rfi Kiswahili

Kisha utekelezwaji wa ahadi za serikali kufanyika kufikia Januari 2025, kutia saini kwa mkataba wa makubaliano kuandaa mashindano utafanyika kati ya sasa hadi February 2024. 

Uwasilishaji wa mipango kufikia Aprili 31 mwaka ujao, lakini pia kila serikali inafaa kuweka kwenye benki dolla elfu 30 ambazo ni mojawapo ya kigezo cha kuandaa AFCON kuwa lazima mwandalizi awe na dola elfu 90. Mchango huo wa kila taifa unafaa kufanyika kufikia tarehe 15 Januari 2025. 

Kikao kilipendekeza muundo wa usimamizi ambapo kamati za kuendesha mashindano zinazojumuisha mawaziri watatu, makatibu watatu na marais watatu wa shirikisho zote, zitakua chini ya serikali zote tatu. Kisha kwenye ngazi ya taifa, kamati ya uratibu itasimamia vikundi kumi vya kazi kabla ya kuripoti katika ngazi ya Afrika Mashariki.   

Vikundi vya kazi ni nini?  

Hivi ni vikundi vidogo vitakavyojukumika ndani na nje ya uwanja. Vikundi hivi vitajumuisha;  

  1. Usalama na afya 
  2. Miundo misingi ya soka, mipango ya urithi na uendelevu 
  3. Vyombo vya habari vya mawasiliano na mauzo ya mashindano 
  4. Utalii, ushiriki wa raia wa ndani na utangazaji wa mashindano 
  5. Miundombinu ya usafirishaji 
  6. Upangaji wa hafla na shirika la maandalizi 
  7. Mapokezi, namna ya kuhamia sehemu tofauti na itifaki 
  8. Ushiriki wa mashabiki na uzoefu kwa kujumuisha teknolojia 
  9. Masuala ya kisheria, fedha na mikataba 
  10. Ushirikiano wa kikanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki 
KATIBU MKUU WA WIZARA YA MICHEZO NCHINI KENYA PETER TUM
KATIBU MKUU WA WIZARA YA MICHEZO NCHINI KENYA PETER TUM © rfi Kiswahili

Katibu mkuu wa wizara ya michezo nchini Kenya, Peter Tum na wenzake kutoka Tanzania Gerson Msigwa na mjumbe wa FUFA Rodgers Byamukama kwa kauli moja waliridhika na ramani hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.