Pata taarifa kuu
CECAFA U18

Fainali ya CECAFA U18 kati ya Kenya na Uganda, usalama zaidi kuimarishwa

Kisumu, Kenya – Idadi ya afisa wa polisi na afisa ambao huelekeza mashabiki na wageni mashuhuri uwanjani itaongezwa katika fainali siku ya Ijumaa wiki hii katika mashindano ya CECAFA kwa wavulana walio chini ya miaka 18.

Mlinda lango wa Tanzania Anthony Mpemba akiurukia mpira wa kona katika mechi dhidi ya Kenya 5/12/2023
Mlinda lango wa Tanzania Anthony Mpemba akiurukia mpira wa kona katika mechi dhidi ya Kenya 5/12/2023 © Football Kenya Federation
Matangazo ya kibiashara

Haya ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo la shirikisho za kandanda Afrika Mashariki na Kati, Auka Gecheo.

Katika nusu fainali, tuliona mashabiki wakiingia uwanjani kusherehekea ushindi wa Kenya dhidi ya Tanzania. Hilo haliruhusiwi na FIFA, CAF au FKF. Hatungependa lijirudie kwenye fainali.

CECAFA na FKF iliandaa vikao kadhaa siku ya Jumanne baada ya tukio uwanjani Mambo Leo hadi asubuhi siku ya Jumatano walipoandaa mkutano mwingine wa usalama kuainisha mambo kabla ya fainali.

Mashindano haya yanayohusisha timu nane ambazo ni wanachama wa CECAFA yakifanyika katika miji miwili, Kisumu na kakamega ilio magharibi mwa kenya.
Mashindano haya yanayohusisha timu nane ambazo ni wanachama wa CECAFA yakifanyika katika miji miwili, Kisumu na kakamega ilio magharibi mwa kenya. © CECAFA

Auka amewaomba mashabiki kutoingia uwanjani akisema mashabiki elfu kumi na tano tu (ambao watafika wa kwanza kuanzia mechi ya Tanzania dhidi ya Rwanda saa tano asubuhi kabla ya fainali saa nane mchana) ndio watakaoruhusiwa kuingia uwanjani.

Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya kupunguza mashabiki kupita kiasi, CECAFA ikifafanua mbinu ya kutumia tiketi kujua idadi ya watakaoingia licha ya kuwa hakuna ada ya mashabiki.

“Kaunti ya Kisumu imeruhusu mashabiki kutazama mechi katikati mwa mji kwenye runinga kuu. Mechi hii pia itapeperushwa kwenye runinga nyumbani na mitandao ya kijamii,” alibainisha Auka Gecheo.

“Tunatoa wito kwa umma kudumisha amani na utulivu. Tunafaa kuonesha mfano mzuri ili tuweze kuandaa CHAN na mashindano mengine,” walisisitiza kwa pamoja naibu rais wa FKF, Doris Petra na mjumbe wa FKF kanda ya Nyanza, Joseph Andere.

Nani ataibuka mbabe?

Timu zote zilikamilisha mazoezi Alhamisi mchana huku vikosi vyote vikiwa havina majeraha yoyote.

Tanzania itachuana na Rwanda mapema asubuhi katika uwanja huo kuwania nafasi ya tatu na nne kabla ya Kenya na Uganda kupambania ubingwa baadaye mchana.

 

 

Kocha wa Kenya Salim Babu amesema wakati huu atalenga kushambulia mapema kutafuta mabao ya haraka lakini ametupilia mbali ukubwa wa kimwili wa wachezaji wa Uganda.

Kenya na Tanzania ni timu tofauti. Tutaikabili Uganda tofauti kabisa. Tumewatayarisha wachezaji wetu vizuri kisaikolojia.

Mwalimu Babu aidha amedai hana “shinikizo yoyote kutoka kwa mashabiki wengi wa Kenya kushinda ubingwa huo lakini nawaomba wakuje wengi kama juzi.”

Mlinda lango Ibrahim Wanzala ambaye aliokoa penalti mbili dhidi ya Tanzania amesema bado hajapata kikubwa cha kujivunia.

Kuokoa penalti imepita tayari, sasa ndio kazi inaanza. Nang’ang’ana kufanikiwa katika hatua hii ya mwisho.

Kambi ya Uganda na Tanzania

Uganda waliandaa mashindano ya wavulana walio chini ya miaka 15 mwezi uliopita ila wakapoteza kwenye fainali dhidi ya Zanzibar kupitia mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 katika uwanja wa kiufundi wa FUFA mjini Njeru.

“Hilo pekee ni motisha tosha kushinda ubingwa huu kesho. Tulisikitika sana kukosa kutwaa ubingwa wa U15. Wakati huu tutajaribu kushinda U18,” alisema kocha Morley Byekwaso kwa masikitiko.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda kwenye mazoezi uwanjani Kodiaga jijini Kisumu
Wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda kwenye mazoezi uwanjani Kodiaga jijini Kisumu © FUFA

Aidha kocha Morley anafahamu uzito wa fainali hii kwa wachezaji wake.

Fainali wakati mwingine husababisha wasiwasi kwa wachezaji chipukizi. Lakini tukifanya kama tunavyofanya mazoezini, tutabeba kikombe. Tumewaambia wachezaji wetu wawe na utulivu kutokana na presha ya mashabiki wa Kenya ambao ni wengi sana kwa hivyo lazima tuwe tayari.”

Mchezaji wa Uganda Anguti Louis amewashukuru wakenya kwa malezi mazuri ila ameahidi Uganda itailaza Kenya.

Kenya wanajua wao ndio mabingwa lakini kwetu wao si mabingwa.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania kwenye mazoezi uwanjani Kodiaga jijini Kisumu 7/12/2023
Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania kwenye mazoezi uwanjani Kodiaga jijini Kisumu 7/12/2023 © TFF

Tanzania kwa upande mwingine itachuana na Rwanda kuwania nafasi ya tatu. Kocha wa Tanzania Habibu Kondo ametaja marekebisho watakayofanyia kazi kutoka kwa mchezo dhidi ya Kenya.

Tukiwa na utulivu katika umaliziaji basi tunaweza pata matokeo mazuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.