AFCON: Mali imeilaza Afrika Kusini mabao 2 kwa 0
Nairobi – Timu ya taifa ya Burkina Faso, imeanza vema michuano ya kutafuta ubingwa taji la soka barani Afrika AFCON, inayoendelea nchini Cote Dvoire baada ya kuifunga Mauritania baoa 1 Kwa 0 kupitia mkwaju wa penalti, uliofungwa na Bertrand Traore aliyeipa ushindi timu yake katika dakika ya 96.
Imechapishwa:
Cheza - 01:06
Katika matokeo mengine, Namibia ilipata ushindi wa kihistoria wa bao 1 kwa 0 dhidi ya mabingwa wa zamani Tunisia, huku Mali nayo ikailaza Afrika Kusini mabao 2 kwa 0.
Leo ni zamu ya wawakilishi kutoka Afrika Mashariki, Tanzania itachuana na Morocco katika mechi ya kwanza ya kundi F saa 11 saa za Afrika Mashariki na baadaye DRC itamenyana na Zambia.
Mwandishi wetu Jason Sagini yupo mjini San Pedro, ametuma ripoti ifuatayo…