Pata taarifa kuu
AFCON 2023

CAF imeanzisha uchunguzi dhidi ya Shirikisho la mpira la Morocco na DRC

Korhogo, Cote d'Ivoire – CAF imeanzisha uchunguzi dhidi ya Shirikisho la Soka la Royal Morocco (FRMF) na Shirikisho la Soka la Kongo (FECOFA) kufuatia matukio ya baada ya mechi wakati wa mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cote d'Ivoire 2023 kati ya Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumapili iliyopita uwanjani Laurent Pokou jijini San Pedro. Kusudi ni kutoa mwanga juu ya matukio na kuwaadhibu wale walio na makosa. 

Nahodha wa DRC Chancel Mbemba akimnyoshea kidole kocha wa Morocco Walid Regragui
Nahodha wa DRC Chancel Mbemba akimnyoshea kidole kocha wa Morocco Walid Regragui © FECOFA
Matangazo ya kibiashara

Kocha wa Morocco, Walid Regragui baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo, alienda moja kwa moja dhidi ya Chancel Mbemba aliyekuwa amepiga magoti akiomba baada ya mchezo. Hapo ndipo mkwaruzano ulianzia.

 

Mgogoro huu uliendelea hadi kwenye eneo la wachezaji kuingia uwanjani huku mlinda lango wa Morocco Yacine Bonou, akionekana akijaribu kumvuta nyuma mchezaji mwenzake kutomshambulia Chancel ambaye alipita kuelekea chumba cha kubadilishia mavazi.

Baadaye mitandaoni kulizuka maneno ya ubaguzi wa rangi yaliyoelekezwa kwa Chancel.

Uchambuzi wa Muktadha

Kwenye kanda za video za runinga mechi ikipeperushwa mubashara, nahodha wa DRC anaonekana akitoa ishara ya mfumo wa VAR kuwa ulihakiki penalti waliyopewa DRC kipindi cha kwanza.

Huenda kocha Walid alihisi haikustahili kuwa penalti lakini Mbemba kwenye video anasisitiza kwa ishara mwamuzi kutoka Kenya Peter Waweru Kamaku, alihakiki ni penalti.   

Aidha Chancel alionekana kuchukuwa muda mwingi sana kuenda nje ya uwanja kwa sekunde chache kwa maagizo ya mwamuzi wa kati baada ya kupata jeraha dogo kipindi cha pili. Huenda hili lilitafsiriwa na kocha Walid kama mbinu ya kupoteza muda.

“Namheshimu kocha ambaye ni mtu mkubwa. Kuna video kwenye runinga! Muhimu zaidi, mimi nitakaa kimya, ni bora zaidi. Maneno haya yalitoka kwake. Yeye mwenyewe atazungumza,” Chancel Mbemba baada ya mabishano yake dhidi ya Walid Regragui.

Kocha wa Morocco Walid Regragui kwenye mahojiano na wanahabari
Kocha wa Morocco Walid Regragui kwenye mahojiano na wanahabari © Morocco FA

Kwenye mahojiano na wanahabari baada ya mechi, Walid Regragui alidinda kutoa maelezo kamili ya kisa hicho.

Inatokea katika soka. Namheshimu sana Chancel. Hakuna tatizo kati yangu na Mbemba. Tunasonga mbele.

Walid Regragui na Chancel Mbemba watakwenda mbele ya Kamati ya Nidhamu ya CAF siku ya Alhamisi kujibu maswali juu ya kile kilichotokea kabla na baada ya mchezo.

CAF imesema haitatoa maoni yoyote zaidi kuhusu suala hili hadi uchunguzi utakapokamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.