Pata taarifa kuu

AFCON 2024 : Mambo yakutarajia katika hatua ya 16 bora

Nairobi – Mwenyeji Ivory Coast, DRC, Senegal, Nigeria na Misri ni miongoni mwa timu zilizosalia katika Mashindano, zikilenga kupambana katika hatua ya 16 bora.

Mechi za AFCON 2023 zinaandaliwa nchini Ivory Coast
Mechi za AFCON 2023 zinaandaliwa nchini Ivory Coast REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Michuano ya Kombe la mataifa ya bara Afrika, AFCON baada ya mapumziko ya siku mbili, sasa ni wakati wa hatua ya mtoano raundi ya 16 bora kuanzia leo Jumamosi, 27.01.2024.

Mechi ya kwanza ya itazikutanisha timu mbili zinazokadiriwa kua za kiwango cha wastani, Angola na Namibia.

Namibia vs Angola (Jumamosi, Saa kumi na moja saa za Afrika Mashariki)

Collin Benjamin, kocha wa timu ya taifa ya Namibia
Collin Benjamin, kocha wa timu ya taifa ya Namibia AFP - KENZO TRIBOUILLARD

Angola ilimaliza kileleni wa Kundi D bila kushindwa huku Namibia ikifuzu kama moja ya timu bora zilizopo katika nafasi ya tatu.

Namibia inajivunia fowadi hatari ya Deon Hotto na Peter Shalulile, wakati Mabululu na Gelson Dala wote walio na mabao mawili wakitegemewa na Angola.

Cameroon vs Nigeria

Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon
Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon AFP - KENZO TRIBOUILLARD

Wakati huo huo, mabingwa mara tano Cameroon watachuana na washindi mara tatu Nigeria katika pambano lingine la kusisimua.

Nigeria inajivunia uwepo wa mchezaji bora wa Afrika mwaka uliopita Victor Osimhen huku Cameroon wakijivunia Karl Toko Ekambi aliyefunga bao moja kufikia sasa.

Taarifa njema kwa Simba wasiotikisika ni kua mshambualiaji Vincent Aboubakr amerejea kikosini na uenda akaanza dhidi ya Super eagles ya Nigeria.

Ivory Coast dhidi ya Senegal

Aliou Cissé - Kocha wa timu ya taifa ya Senegal
Aliou Cissé - Kocha wa timu ya taifa ya Senegal AFP - ISSOUF SANOGO

Wenyeji Ivory Coast watacheza dhidi ya mabingwa watetezi Senegal, ambao ndio timu pekee iliyoshinda mechi zote katika hatua ya makundi.

Sadio Mane anaiongoza Senegal kutetea ubingwa wa AFCON huku Ivory coast wakiongozwa na kiungo Seko Fofana akitafuta kunyakua taji la kwanza la Afcon tangu 2015 kwa Tembo wa Cote d’Ivoire.

Kufuatia kufedheheshwa na Equatorial Guinea katika mechi yao ya mwisho ya Kundi A, wenyeji walimtimua Jean-Louis Gasset kabla ya maendeleo yao kuthibitishwa.

The Elephants pia wameshindwa katika juhudi za kutafuta huduma za Herve Renard kocha wao aliyeshinda taji la 2015, na kocha wa muda Emerse Fae sasa atahitaji kuimarisha tena Ivory Coast dhidi ya wapinzani wa kutisha Senegal.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Côte d'Ivoire
Mashabiki wa timu ya taifa ya Côte d'Ivoire AFP - FADEL SENNA

Misri dhidi ya DRC (Jumapili, Saa Mbili usiku, Saa za Afrika Mashariki)

Hadhari ya jeraha la nahodha wa Misri Mohamed Salah yanaweza kuwa makubwa wakati The pharaohswatakapocheza na DR Congo. 

Kando na Salah, vijana wake Rui vitoria wanatarajiwa kumkosa Emam Ashour, baada ya kiungo huyo kupata mshtuko katika mazoezi wiki hii.

DR Congo walifanikiwa kupata sare katika mechi zao zote tatu za makundi moja ikiwa ni dhidi ya Morocco waliofika hataua ya nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2022.

Mmorocco Achraf Hakimi na Mkongo Silas Katompa Mvumpa, wote wawili waliofunga mabao wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024.
Mmorocco Achraf Hakimi na Mkongo Silas Katompa Mvumpa, wote wawili waliofunga mabao wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024. © AFP / SIA KAMBOU

Equatorial Guinea dhidi ya Guinea (Jumapili, Saa Kumi na Moja, Saa za Afrika Mashariki)

Wakati nyota wenye majina makubwa wameshindwa kufunga magoli mengi katika michuano hii, Emilio Nsue wa Equatorial Guinea anaongoza kwa magoli matano.

Nsue amekua mchezaji wa kwanza katika kipindi cha miaka 13 kufunga hat-trick ya AFCON katika ushindi wa 4-2 wa nchi yake dhidi ya Guinea - Bissau na kuongeza mengine mawili dhidi ya Ivory Coast.

Guinea pia ina uthabiti wa hali ya juu, na kutinga hatua ya 16 bora kwa mchuano wa nne mfululizo.

Mauritania vs Cape Verde (Jumatatu, Saa kumi na Moja saa za Afrika Mashariki)

Mauritania watachuana na Cape Verde (Jumatatu, 17:00 saa za Afrika Mashariki).

Kama zawadi yao kwa kuwashinda mabingwa wa 2019 Algeria na kusajili ushindi wao wa kwanza kabisa katika fainali hizi.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Cape Verde
Wachezaji wa timu ya taifa ya Cape Verde © AFP - FRANCK FIFE

Simba wa Chinguetti ndiyo timu pekee iliyo na nafasi ya chini ya 1% ya kunyakua ubingwa, kwa mujibu wa wataalamu wa takwimu Opta. 

Kocha Amir Abdou ameiga mafanikio aliyopata kwa kuipeleka Comoro hadi hatua ya 16 bora mwaka wa 2021.

"Ni ajabu tunayopitia. Niliwaambia wachezaji kwamba waliandika historia ya Mauritania," alisema Abodu.

Wapinzani wao Cape Verde na wanajivunia kiwango bora kilichowawezesha Kuzishinda Ghana na Msumbiji na kuongoza kundi lao.

Morocco ndiyo timu iliyoorodheshwa zaidi barani Afrika, ikiwa katika nafasi ya 13 duniani, lakini taji lao pekee la bara lilikuja mwaka 1976.

Mali vs Burkina Faso ( Saa Kumi na Moja EAT)

Siku ya Jumanne, Mali watamenyana na Burkina Faso. The Eagles waliendeleza rekodi yao ya kutoshindwa katika hatua ya makundi hadi michezo 10 katika michuano minne.

Burkina Faso wanajivunia nafasi bora katika mashindano ya AFCON ya kumaliza kama mshindi wa pili mwaka 2013 na nusu fainali 2017 pamoja na 2021.

Jukumu lao sasa ni kuboresha rekodi yao ya hivi majuzi ya kupoteza nane katika mechi 10 dhidi ya Mali, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa mabao 3-1 katika hatua ya makundi kwenye fainali za Afcon za 2004.

Morocco vs Afrika Kusini  (Jumanne, Saa Mbili usiku EAT)

Kocha wa Morocco Walid Regragui anatazamiwa kurejea kwenye eneo la ufundi ili kuona Atlas Lions ikicheza na Afrika Kusini .

Hii ni baada ya Walid kupigwa marufuku na kukata rufaa. 

Morocco ndiyo timu iliyoorodheshwa zaidi barani Afrika, ikiwa katika nafasi ya 13 duniani, lakini taji lao pekee la bara lilikuja mwaka 1976.

Fiston Mayele, mchezaji wa DRC akikabiliana na mchezaji wa Morocco Achraf Hakimi wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024.
Fiston Mayele, mchezaji wa DRC akikabiliana na mchezaji wa Morocco Achraf Hakimi wakati wa mechi kati ya Morocco na DRC mjini San Pedro, Januari 21, 2024. © AFP / SIA KAMBOU

Achraf Hakimi na Hakim Ziyech pamoja na Sofyan Amrabat ni baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa watakao iongoza timu ya Morocco.

Afrika Kusini iliishinda Namibia mabao 4-0 katika mchezo wao wa pili ushindi wao mkubwa kuwahi kutokea wa Afcon.

Hakuna timu ya kusini mwa Afrika katika shirikisho la Cosafa iliyotinga fainali ya AFCON tangu Zambia iliposhinda kwa kushtukiza mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.