Pata taarifa kuu

AFCON: Mechi za nusu fainali, DRC kucheza dhidi ya Ivory Coast

Nairobi – Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika, inachezwa leo Jumatano usiku.

Wachezaji wa timu ya taifa ya DRC wakati wa mechi dhidi ya Guinea
Wachezaji wa timu ya taifa ya DRC wakati wa mechi dhidi ya Guinea © FMM
Matangazo ya kibiashara

Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Nigeria na Afrika Kusini, kuanzia saa Mbili usiku mjini Bouake.

Mataifa haya mawili yana ushindani wa muda mrefu katika mchezo wa soka.

Nyota wa Nigeria, Victor Osimhen ambaye wiki iliyopita alipata jeraha amepona na atacheza kwenye ya leo.

Victor Osimhen amepona jeraha na atacheza mechi ya leo dhidi ya Afrika Kusini
Victor Osimhen amepona jeraha na atacheza mechi ya leo dhidi ya Afrika Kusini AP - Sunday Alamba

Mchezo huu pia umezua mvutano wa kidiplomasia, Balozi wa Nigeria nchini Afrika Kusini, amewaambia raia wa nchi yake kuwa makini leo usiku, iwapo wataishinda Afrika Kusini ili kuepuka sintofahamu inayoweza kutokea.

Katika hatua nyingine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nayo itacheza na wenyeji Ivory Coast jijini Abidjan.

Wachezaji wa timu ya taifa ya RDC
Wachezaji wa timu ya taifa ya RDC AP - Sunday Alamba

Wachezaji wa Leopard katika mechi ya leo watavalia vitambaa vyeusi, kuomboleza na raia wengine wa nchi yao kutokana na mauaji ya watu huko Mashariki mwa DRC na kuomba amani.

Washindi wa mechi za leo, watakutana kwenye fainali siku ya Jumapili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.