Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

"Jumanne Kuu" kwa kura za mchujo Marekani

Ikiwa imesalia mwezi mmoja na nusu kabla ya kuhitimisha kura za mchujo nchini Marekani, mamilioni ya Wamarekani wametolewa wito kuitikia zoezi hilo Jumanne hii katika majimbo matano yanayosalia.

Hillary Clinton na Donald Trump wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kura za mchujo katika majimbo matano yanayosalia kwa «Jumanne Kuu», Aprili 26, 2016. 2016.
Hillary Clinton na Donald Trump wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kura za mchujo katika majimbo matano yanayosalia kwa «Jumanne Kuu», Aprili 26, 2016. 2016. REUTERS/David Becker/Nancy Wiechec/Files
Matangazo ya kibiashara

Hillary Clinton ana matumaini ya kushinda kwa kishindo na Donald Trump ameapa kuwabwaga kabisa washindane wake.

Wadadisi wanasema wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda kura hizo za mchujo ikiwa ni pamoja na Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic, wala bilionea Donald Trump kutoka chama cha Republican hawawezi kufikisha kuanzia Jumanne hii idadi kubwa inayohitajika ya wajumbe kwa uteuzi wa vyama vyao.

Lakini idadi kubwa ya wajumbe ambayo inatafutwa sasa itawakutanisha kwa karibu kwa lengo lao, hasa Hillary Clinton ambaye tayari anaongoza kwa kiasi kikubwa dhidi ya mshindani wake, Seneta Bernie Sanders.

Majimbo matano ya Pwani ya Mashariki ya Marekani (Maryland, Delaware, Pennsylvania, Connecticut na Rhode Island) yanaandaa kura za mchujo za vyama vya Democratic na Republican. Uchunguzi unaonyesha kuwa Donald Trump ataibuka mshindi, kutokana na ushindi alioupata dhidi ya washindani wake katika jimbo la New York wiki iliyopita.

Upande wa chama cha Democratic, Hillary Clinton anashikilia nafasi nzuri katika majimbo makubwa mawili, Pennsylvania na Maryland, ambayo ina watu wachache kutoka jamii ya watu weusi, lakini kisiasa Bii Hillary Clinton ni maarufu sana kutokana na wadhifa alioshikilia miaka iliyopita kama Waziri wa mashauriano ya Kigeni wa Marekani

Kwa upande wa Donald Trump, umuhimu siyo tu kushinda kura za mchujo ziliyobaki, lakini kushinda kwa asilimia kubwa zaidi. Anahitaji kunyakua 58% ya wajumbe ambao bado wanatafutwa ili aweze kuteuliwa kama mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican. Kwa sasa ana wajumbe 846, na anahitaji kuwa na wajumbe wengi hadi kufikia 1,237.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.