Pata taarifa kuu
UKRAINE

Rais Poroshenko kuapishwa leo mjini Kiev

Rais mteule wa Ukraine Petro Poroshenko anatarajia kuapishwa leo Jumamosi, huku kukiwa na mwanga wa matumaini kwa ufumbuzi wa mgogoro ambao umechafua taifa hilo dhidi ya jirani yake mkubwa Urusi.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko (wa pili kushoto),Kansela wa Ujerumani  Angela Merkel (kushoto)na rais wa Urusi  Vladimir Putin wakiwa Normandy Ufaransa jana Ijumaa
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko (wa pili kushoto),Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto)na rais wa Urusi Vladimir Putin wakiwa Normandy Ufaransa jana Ijumaa Reuters/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo mpya wa Ukraine ataapishwa ndani ya bunge mjini Kiev siku moja baada ya kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin,Nchini Ufaransa, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya vita ya pili ya dunia maarufu kama D Day.

Putin na Poroshenko kwa pamoja walitoa wito wa kusitisha mapigano kusini mwa Ukraine hatua ambayo imeonekana kuwa mwanzo wa kupata mpenyo katika mgogoro ambao umetia sumu mahusiano ya Moscow na nchi za Magharibi.

Akizungumza katika televisheni ya Ukraine muda mfupi baada ya kukutana,Poroshenko amesema mazungumzo yameanza, na kwamba ni jambo jema, na kuongeza kuwa mwakilishi wa Urusi atasafiri kwenda Ukraine kwa ajili ya mazungumzo kesho Jumapili huku kukiwa na hatua ya kwanza baina ya kuelekea kutatua tofauti zao.

Poroshenko mwenye umri wa miaka 48 alichaguliwa kwa asilimia 54 .7 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa Mei 25 na sherehe za kuapishwa kwake zitahudhuriwa na viongozi mashuhuri duniani akiwemo makamu wa rais wa Marekani Joe Biden na rais wa umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy.

Poroshenko atachukua rasmi madaraka na kumrithi mtangulizi wake Viktor Yanukovych, ambaye aliondolewa madarakani mwezi Februari baada ya mapigano na umwagaji damu kuenea katika mji wa Kiev na ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Urusi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.