Pata taarifa kuu
Ukraine-Mapigano

Mji wa Marioupol warejea mikononi mwa vikosi vya serikali ya Ukraine

Vikosi vya jeshi la Ukraine vimefaulu Ijumaa hii kuurejesha kwenye himaya yaje mji wa Marioupol baada ya mapigano makali usiku kucha yalio sababisha wanajeshi 4 kujeruhiwa wakati huu rais Petro Porochenko akiaumuru kuundwa kwa utawala wa eneo la Donetsk.

mwajaeshi wa serikali ya Ukraine
mwajaeshi wa serikali ya Ukraine Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Porochenko amesema kufuatia ushindi mkubwa wa vikosi vyake, hali imerejea kuwa tulivu katika mji wa Marioupol, bandari ilipo kusini mashriki mwa Ukraine ambpo wanaeshi watu zaidi ya laki tano.

Rais Porochenko ametowa wito kwa Gavana wa Jimbo la Donetsk Serguii Tarouta kuunda haraka uongozi wa muda katika mji wa Marioupol. Mji wa Donetsk unakaliwa takriban miezi miwili sasa na kundi la watu wanaodai mjitango na Ukraine na ambapo wameweka makao makuu ya kundi lao.

Mpigaaji wa waasi katika kituo kilichoachwa na jeshi la ukraine cha Chervonopartyzansk,  7 juin 2014.
Mpigaaji wa waasi katika kituo kilichoachwa na jeshi la ukraine cha Chervonopartyzansk, 7 juin 2014. REUTERS/Shamil Zhumatov

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Arsen Avakov amesema katika taarifa yake kwamba Askari wanne wa Ukraine wamejeruhiwa katika mapigano hayo mapema leo asubuhi mjini Marioupol, huku waasi wakipata pigo kubwa kwa kupoteza idadi kubwa ya wapiganaji wao.

Awali taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani iliarifu askari wawili ndio waliojeruhiwa. Askari maalum wa Ukraine wamefaulu kuondowa vizuizi vilivyowekwa na wapiganaji na hatimaye kupeperusha kwa nyingine tena bendera ya Ukraine.

Jeshi la Ukraine linaendesha tangu takriba miezi miwili operesheni ya kurejesha miji iliotekwa na kuwa mikononi mwa kundi la watu wanaodai mjitengo, mapigano ambayo tayari ymegharimu maisha ya watu 270.

Upande wake waziri wa ulinzi wa Ukraine amesema kumeshuhudiwa mapigano makali karibu na mpaka na Urusi katika vitongoji cha Snijne na Stepanivka jimbo la Donetsk.
Waziri wa ulinzi ameendelea kuwa wamefaulu kuharibu silaha za waasi waliokuwa katika msafara wa magari wakitokea nchini Urusi, na baada ya kushambulia msafara huo kwa ndege, askari wa Ukraine walitua kutoka hewani huku waasi wakipata pigo kubwa kwa kupoteza zaidi ya wapiganaji kumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.