Pata taarifa kuu
UFARANSA-GAZA-Vita vya kwanza vya dunia-Usalama

Ufaransa : Hollande ataka vita katika ukanda wa Gaza vikomeshwe

Rais wa Ufaransa, François Hollande, ametolea wito viongozi mbalimbali wa matiafa ya Ulaya wanaoshiriki maadhimisho ya miaka 100 tangu vita vya kwanza vya duni kufanya kila waliwezalo ili kukomesha mauaji yanoendelea kushuhudiwa katika ukanda wa Gaza.

Kwa mara ya kwanza Ufaransa inatumia neno "mauaji dhidi ya wapalestina" yanayotekelezwa na Israeli.
Kwa mara ya kwanza Ufaransa inatumia neno "mauaji dhidi ya wapalestina" yanayotekelezwa na Israeli. REUTERS/Laurent Dubrule
Matangazo ya kibiashara

“Wakati ninapoona hali inayoikabili jamii ya wakristo waishio Iraq, waliyo wachache nchini Syria, na mauaji ya kila kukicha. Hali pia inayojiri katika ukanda wa Gaza, ambapo wapalestina wanaendelea kuuawa kiholela kwa kipindi chote hiki cha siku 26 ncha machafuko. Kwa hiyo tunapaswa kuchukua msimamo”, amesema rais wa Ufaransa.

Ni kwa mara ya kwanza Ufaransa inalani machafuko hayo yanayoendelea katika ukanda wa Gaza, na ni mara ya kwanza pia taifa hilo kutumia neno "mauaji dhidi ya wapalestina", yanayotekelezwa na Israeli.

Maadhimisho hayo yalianza jumatatu wiki hii katika mji wa Liège, nchini Ubelgiji.

Viongozi barani Ulaya wamekusanyika katika mji huo kuadhimisha miaka mia moja tangu uvamizi dhidi ya Ubelgiji uliotekelezwa na askari wa Ujerumani wakati wa vita vya kwanza vya dunia.

Sherehe hizo zimeadhimishwa chini ya kauli mbiu ya “Amani , umoja na demokrasia barani Ulaya”, ambavyo vinatakiwa kuendelezwa na kuboreshwa amesema mfalme Philippe wa Ubelgiji na mwenyeji wa maadhimisho hayo .

Kwa upande wake rais wa Ujerumani Joachim Gauck ambaye nchi yake ndiyo iliyotekeleza uvaamizi huo hakuomba radhi katika hotuba yake kwa niaba ya nchi yake na badala yake ameomba wananchi wa nchi hizo kutumia fursa hiyo kupata funzo ya kihistoria.

Nchi themanini na tatu ambazo zimeshiriki katika vita vya kwanza vya dunia zimealialikwa katika maadhimisho hayo ambapo marais na wafalme wa nchi kumi ndio walifanya safari hiyo akiwepo Felipe mfalme wa Uhispania ambaye kwake ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi yake na wengine kuwakilishwa.

Mji wa Liège uliwekwa chini ya ulinzi mkali kwa ajili ya tukio hilo ambapo watu wengi wameshuhudia maadhimishi hayo kwa njia ya televisheni na wavuvi kumbwa kubaki makwao hadi tamati ya maadhimisho hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.