Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI

Mzozo wa Ukraine;Mataifa ya Magharibi yalaani uvamizi wa Urusi

Mataifa ya magharibi yamelaani Uamuzi wa Urusi kutuma msaada wa zaidi ya malori mia moja katika eneo lenye mapigano mashariki mwa Ukraine bila kibali kusubiri kumaliza kwa ukaguzi.

Baada ya wiki moja ya kuzuiwa ujumbe wa Urusi umeanza kuingia Ukraine hatua ambayo inapingwa na mataifa ya magharibi
Baada ya wiki moja ya kuzuiwa ujumbe wa Urusi umeanza kuingia Ukraine hatua ambayo inapingwa na mataifa ya magharibi REUTERS/Alexander Demianchuk
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya na Marekani zilitoa wito kwa Urusi kujiondoa huko kwa kile walichokiita uwepo wa Urusi unakiuka utawala wa Ukrine,NATO inaona kuwa hatua hiyo itachochea mgogoro huo.

Urusi imekanusha taarifa hizo na kusema suala la kucheleweshwa zaidi halikubaliki.
Malori yaliyowasili tayari yapo katika mji unaoshikiliwa na waasi Luhansk.

Umoja wa mataifa UN uliitisha mkutano wa dharura kujadili hatua hiyo ya urusi ambayo Ukraine imeiita ni uvamizi.

Wachambuzi wa siasa wanaokuwa ni jambo linalo shangaza kwakuwa msafara huo umesubiriwa kwa muda mrefu huku kukiwa na maswali chungu nzima kutaka kujuwa iwapo ni misaada ya kibinadamu kweli au la.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.