Pata taarifa kuu
Ukraine-Urusi-diplomasia

Kansela Angela Merkel azitaka Urusi na Ukraine kusitisha mapigano

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameshinikiza usitishwaji mpya wa mapigano katika mazungumzo yake na Rais wa Ukrainian Petro Porochenko kuhusu mgogoro kati ya Urusi na Ukraine hapo jana, wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru leo Jumapili na msafara tata wa misaada kutoka Urusi ukiripotiwa kurejea kwao.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa na rais wa Ukraine Petro Poroshenko 23 Agosti 2014
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa na rais wa Ukraine Petro Poroshenko 23 Agosti 2014 RFI
Matangazo ya kibiashara

Merkel kiongozi wa Magharibi mwenye ushawishi mkubwa amezuru taifa hilo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa kwa mgogoro huo ziara ambayo pia inakuja kabla ya mkutano muhimu utakao wakutanisha kwa mara ya kwanza Rais wa Ukraine na wa Urusi sambamba na viongozi wa juu wa Umoja wa Ulaya Jumanne ijayo.

Hofu iliongezeka kwa kiwango kikubwa siku ya Ijumaa baada ya Kremlin kupeleka kile inachodai ni malori ya misaada kwenye ngome waasi ya Lugansk hatua ambayo Kiev imeeita uvamizi.

Wakati wa ziara yake kansela Merkel ametoa wito kwa Urusi na Ukraine kusitisha mapigano na kuimarisha udhibiti mipakani ili kusaidia kukomesha miezi minne ya mapigano ya kikatili kati ya waasi wanaounga mkono Urusi na wanajeshi wa serikali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.