Pata taarifa kuu
UHISPANIA-Ebola-Afya

Uhispania: muuguzi ambukizwa virusi vya Ebola

Muuguzi mmoja raia wa Uhispania amebainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola anaodaiwa kuwa aliambukizwa na wagonjwa aliyekua akiwahudumia kutoka nchi za Afrika Magharibi.

Padiri Garcia VIejo, raia wa Uhispania alieambukizwa virusi vya Ebola nchini Sierra Leone, aliwasili Uhispania Septemba 22 mwaka 2014. Muuguzi aliemuhudumia amelazwa hospitali baada ya kubainika kuwa na virusi vya Ebola.
Padiri Garcia VIejo, raia wa Uhispania alieambukizwa virusi vya Ebola nchini Sierra Leone, aliwasili Uhispania Septemba 22 mwaka 2014. Muuguzi aliemuhudumia amelazwa hospitali baada ya kubainika kuwa na virusi vya Ebola. REUTERS/Ministry of Defence/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Muuguzi huyo ni mtu wa kwanza kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchi Uhispania.

Muuguzi huyo ni miongoni mwa kikosi cha madakatri nchini Uhispania waliowatibu wamisionari wawili walioambukizwa virusi vya Ebola katika nchi ya Sierra Leone na baadaye kurejeshwa nyumbani kwao Uhispania.

Mmoja kati ya wanadini hao Uhispania, Manuel Garcia Viejo, alirejeshwa nchini Uhispania Septemba 21 baada ya kubainika kua anavirusi vya Ebola na alifariki mwishoni mwa mwezi uliyopita.

Kulingana na chanzo cha hospitali, muuguzi huyo alimuhudumia, Garcia Viejo mara mbili, wakati wa kumfanyia vipimo na alipofariki. Hali hiyo ilitosha kwa muuguzi huyo wa hospitali Carlos Tercero, mwenye umri wa miaka 44 kuambukizwa virusi vya Ebola.

Wakati huo huo, tahadahri zimetolewa na Wizara ya afya ikiwasihi wakaazi wa mji kuu wa Uhispania Madrid kuwa makini, baada ya hali hiyo kutokea.
Waziri wa afya, Ana Matao amekutana na wadau wote katika sekta ya afya, akibaini kwamba hatua zinazohitajika zimechukuliwa ili kuhakikisha kwamba usalama umeimarishwa kwa wafanyakazi wa hospitali mbalimbali, hususan madaktari na wauguzi.

Kwa sasa uchunguzi umeanzishwa kwa wauguzi na madaktari waliokua wakishirikiana na muuguzi huyo aliyebainika kuwa na virusi vya Ebola, ili kujua iwapo wameambukizwa virusi hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.