Pata taarifa kuu
UTURUKI-WAKIMBIZI-IRAQ-SYRIA

Wakurdi 200,000 wakimbilia Uturuki

Uturuki ni nchi ya kwanza kuwapokea na kuwapa hifadhi wakimbizi wa Syria, ambapo wakimbizi milioni 2 wanaishi katika kambi aidha katika nyumba walikopewa hifadhi.

Wakimbizi wa Kikurdi kutoka Syria katika mpaka na Uturuki. wameukimbia mji wa Kobane. Sepemba 27 mwaka 2014.
Wakimbizi wa Kikurdi kutoka Syria katika mpaka na Uturuki. wameukimbia mji wa Kobane. Sepemba 27 mwaka 2014. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Tangu kundi la wapiganaji wa Dola la kiislam lilipoanza mashambulizi na kuyateka baadhi ya maeneo nchini Syria na Iraq mwezi Agosti, Uturuki imekua ikiwapokea wakimbizi kutoka Syria na Iraq. Idadi hiyo ya wakimbizi kutoka Syria na Iraq imekua ikiongezeka siku baada ya siku.

Takwimu zilizotolewa na Idara ya kutatua migogoro na kukabiliana na majanga ya asili (AFAD), imebaini kwamba Wakurdi 200,000 walikimbilia Uturuki baada ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam kuanzisha mashambulizi na kuyashikilia baadhi ya maeneo.

Hata hivyo, takwimu hizi pengine ziko chini ya ukweli wa mambo, kutokana na wakimbizi wengi ambao wamekua wakipenya na kuingia usiku kwa kujificha nchini Uturuki. Wakimbizi hao wanaojificha kwa kuingia usiku wanakadiriwa kufikia idadi ya watu 50,000.

Ingawa wakimbizi hao wanapokelewa na manispaa pamoja na raia wa vijiji mbali mbali, wakimbizi hawa hawatazamwi kwa jicho la mapenzi na viongozi wa Uturuki, ambao hawakuwahi kuwashughulikia wakimbizi kutoka jamii ya Yezidis wakati wa uvamizi wa mji wa Sinjar mwezi Agosti mwaka 2014. Angalau Wakurdi 100,000 kutoka jamii ya Yezidis waliweza kuishi nchini Uturuki lakini kinyume cha sheria na chini ya ulinzi wa manispaa za jiji za kikurdi kusini mwa Uturuki .

Katika mikoa jirani ya Kobane, hususan Maras, zaidi ya siku kumi zilizopita hata mwishoni mwa wiki iliyopita katika jimbo la Urfa, wakuu wa mikoa wamesema hawapendelei kuona wanarudi kupokea wakimbizi wapya wa Kikurdi katika katika mikoa yao.

Wakuu hao wa mikoa wamekataa katu katu wakimbizi hao kuhamishwa katika kambi mpya ziliyojengwa hivi karibuni.Wao kumwagwa au kukataliwa ufungaji yao katika makazi mapya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.