Pata taarifa kuu
UFARANSA-Vyombo vya habari-Mkutano-Diplomasia

Hollande akiri kushirikiana kimataifa

François Hollande ameendesha mkutano na waandishi wa habari uliyodumu masaa mawili, akijibu maswali ya waandishi wa habari wa Ufaransa na wale wa kigeni Alhamisi Februari 5.

François Hollande amefanya mkutano wa tano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Champs Elysee, Alhamisi Februari 5 mwaka 2015.
François Hollande amefanya mkutano wa tano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Champs Elysee, Alhamisi Februari 5 mwaka 2015. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umefanyika mwezi mmoja baada ya Ufaransa kushuhudia mfululizo wa mashambulizi. Rais Hollande ameelezea nia yake ya kurefusha " mtazamo wa Januari 11" pamoja na kuchukua baadhi ya hatua.

Rais wa Ufaransa ameonekana kuwa mkali kuhusu faili ya Ukraine, ambapo ametangaza kufanya ziara ya ghafla Alhamisi alaasiri wiki hii mjini Kiev, pamoja na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, na baadae mjini Moscow Ijumaa wiki hii.

 Ufaransa inataka kuepusha vita nchini Ukraine lakini " fursa ya kidiplomasia haiwezi kupanuliwa kwa muda usiojulikana." Hayo ndio François Hollande ametangaza Alhamisi Februari 5 mbele ya waandishi wa habari wa Ufaransa na wale wa vyombo vya habari vya kimataifa waliokua wamekusanyika katika Ikulu ya Champs Elysée.

Ziara hiyo ya ghafla ya viongozi hao wawili nchini Ukraine inaonekana kama jaribio la mwisho la kufikia ufumbuzi kupitia mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine. François Hollande na Angela Merkel watakutana na rais wa Ukraine Petro Poroshenko leo alhamisi alaasiri au jioni.

Wawili hao watajielekeza Ijumaa wiki hii mjini Moscow kukutana na rais wa urusi Vladimir Putin. Kama alivyoeleza François Hollande katika mkutano na vyombo vya habari, lengo ni kuwasilisha pendekezo jipya kwa ajili ya udhibiti wa machafuko ambayo yanaendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine. François Hollande hakutoa maelezo zaidi juu ya maudhui ya pendekezo hilo.

Alipoulizwa kuhusu suala la uwezekano wa kuipa Kiev silaha, François Hollande amesema asingeweza kuingia katika mjadala huo, akimaanisha kuwa, Ufaransa haina nia ya kuipa silaha Ukraine.

" Njia pekee ya kidiplomasia ndio bado inapewa kipaumbele na kwa hio Paris na Berlin wamejitenga na msimamo huo wa Washington kwa sababu Marekani inafikiriwa kutoa vifaa vya kijeshi kwa kupambana na waasi wanaotaka kujitenga katika maeneo ya mashariki", amesema Hollande.

Hata hivyo, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerryyuko ziarani mjini Kiev kujadili faili hiyo muhimu.

Nguvu zaidi katika Mashariki ya Kati na Afrika

Suala jingine la kimataifa: vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. "Mafanikio" ya muungano ya kurejesha nyuma wanajihadi nchini Iraq " yanaenda kwa mwendo wa kinyonga", amekubali Francois Hollande, huku kakihakikisha kwamba Ufaransa ilikuwa " ikifanya kazi yake kwa kutumia nguvu ya kiwango cha juu." Akihojiwa kuhusu uwezekano wa kupanua mashambulizi ya angani ya Ufaransa kutoka Iraq hadi Syria, rais hollande amesema suala hilo haliwezekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.