Pata taarifa kuu
UFARANSA-UBELGIJI-SHAMBULIO-USALAMA

Shambulizi la Thalys: mtuhumiwa akana dhamira ya kigaidi

Ayoub al-Khazzani bado anaendelea kusikilizwa katika makao makuu ya SDAP, kitengo cha polisi kinachopambana na Ugaidi katika mji wa Levallois-Perret.

Treni ya mwendo kasi katika kituo cha treni cha Midi mjini Brussels, Desemba 8 mwa 2014.
Treni ya mwendo kasi katika kituo cha treni cha Midi mjini Brussels, Desemba 8 mwa 2014. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Morocco ambaye amewajeruhi Ijumaa wiki iliyopitaabiria abiria wawili katika treni ya mwendo wa kasi (Thalys) amekanusha kuwa alikua akiishi nchini Syria, lakini Idara ya Ujasusi ya Uhispania imethibitisha.

Baada ya siku mbili akiwa chini ya ulinzi, Ayoub al-Kazzani pia amekanusha nia yoyote ya kigaidi. Mtuhumiwa huyo anaweza kuendea kuwa chini ya ulinzi hadi Jumanne wiki hii.

Mtu dhaifu na mwenye uchovu, ameshangaa kusikia kuwa anatuhumiwai kuhusika na kitendo cha kigaidi kitendo: huu ndio mtazamo wa Sophie David, mwanasheria wa Ayoub al-Khazzani. " Ameshangaa kusikia anakabiliwa na tuhuma za ugaidi. Nilijarubu kumuuliza iwapo ilikua jaribio la mauaji alinijibu hapana kwa sababu risasi zilizosikika. amesema kuwa bunduki aina ya Kalashnikov aliokua nayo haikuweza kufanya kazi alikabiliwa mara moja kabla hajafyatua risasi ", amesema mwanasheria wa mtuhumiwa.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake, huenda kitendo chake kilitokana na nia ya kuwaibia abiria pesa zao. El-Khazzani huenda katika bustani ya mji wa Brussels aliokota kwa bahati mbaya sanduku lilokuwemo bunduki ya aina ya Kalashnikov na simu. Naye alikuwa na wazo la kuitumia kwa kujipatia na kuwaibia abiria waliokua katika treni ya mwendo wa kasi iliokua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Paris.

" Anasema kwamba aligundua sanduku ikiwemo silaha na simu, hasemi kama ni bunduki aina ya Kalashnikov , sanduku ambayo ilikua ilifichwa katika bustani, ilio karibu na kituo cha treni cha Midi mjini Brussels. Kisha alichukua silaha hiyo na kuanza kuzitumia katika treni, ili aweze kuwaibia pesa abiria, huo ndio utetezi wake ", amema mwana sheria wa Ayoub al-Khazzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.