Pata taarifa kuu
UFARANSA-UBELGIJI-SHAMBULIO-USALAMA

Hali ya hatari yaongezwa muda Ufaransa

Hali ya hatari iliongezwa muda na kuimarishwa imeanza kutekelezwa Jumamosi nchini Ufaransa, wiki moja baada ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Wanajeshi wa kipiga doria katika katika mtaa wa kibiashara wa Brussels, Novemba 21, 2015.
Wanajeshi wa kipiga doria katika katika mtaa wa kibiashara wa Brussels, Novemba 21, 2015. JOHN THYS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo Brussels imewekwa katika hali kubwa ya tahadhari kutokana na "hatari ya kutokea kwa mashambulizi" kwa kutumia "silaha na mabomu".

Watuhumiwa saba kati ya nane waliokamatwa Jumatano wakati polisi walipoendesha operesheni katika eneo la Saint-Denis, kaskazini mwa jiji la Paris, wamechiwa Jumamosi. Mtu aliyemuhifadhi katika Abdelhamid Abaaoud katika ghorofa anaendelea kuwekwa chni ya ulinzi. Abdelhamid Abaaoud anatuhumiwa kuandaa mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya 130 Novemba 13 jijini Paris.

Jawad Bendaoud aliliambia shirika la habri la Ufaransa la AFP muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake, kuwa aliwasaidia watu wawili kutoka Ubelgiji kwa kuwapa hifadhi katika ghorofa lake.

Nchini Ubelgiji, viongozi wametangaza usiku tahadhari ya kigaidi kwa kiwango cha juu kwa mkoa Brussels. Waziri mkuu Charles Michel, ambaye ameitisha Jumamosi asubuhi kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa, amebaini "hatari ya kutokea kwa mashambulizi ambayo yangitekelezwa na watu wenye silaha na vilipuzi katika maeneo kadhaa ya mji mkuu."

"Tishio lipo na ni kubwa", Waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders, ameongeza.

Wakazi wa mji wa Brussels wametakiwa kuepuka matamasha, sherehe kubwa, vituo vya treni na viwanja vya ndege, usafiri wa umma na maeneo ya biashara yanayotembelewa na watu wengi. Usafiri wa treni za mwendo kasi umesitishwa Jumamosi kwa "tahadhari" na tamasha la Johnny Hallyday lililokua linatarajiwa leo Jumamosi jioni katika mji mkuu wa Ubelgiji limefutwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.