Pata taarifa kuu

Shirika la misaada nchini Ufaransa linahofu kuelekea Michezo ya Olimpiki

Shirika la kujitolea kuhusu maji nchini Ufaransa, limetoa tahadhari kuhusu uchafuzi wa mazingira katika mto Seine, wakati huu zikiwa zimebaiki siku 100 kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki, mto huo ukitarajiwa kutumika na waogeleaji.

Pete za Olimpiki zimepangwa kwenye uwanja wa Trocadero unaotazamana na Mnara wa Eiffel, siku moja baada ya tangazo rasmi kwamba Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya 2024 itakuwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, Ufaransa, Alhamisi, Septemba 14, 2017. Paris itakuwa mwenyeji. Michezo ya Olimpiki ya Majira ya 2024 na Los Angeles itaandaa Michezo ya 2028.
Pete za Olimpiki zimepangwa kwenye uwanja wa Trocadero unaotazamana na Mnara wa Eiffel, siku moja baada ya tangazo rasmi kwamba Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya 2024 itakuwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, Ufaransa, Alhamisi, Septemba 14, 2017. Paris itakuwa mwenyeji. Michezo ya Olimpiki ya Majira ya 2024 na Los Angeles itaandaa Michezo ya 2028. AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Surfrider Foundation imesema ilikuwa imechambua vipimo vya miezi sita wakati wa msimu wa baridi vilivyofanywa maabara na ikahitimisha kuwa maji ya mto huo yalisalia kuwa machafu na hatari.

Katika barua yake ya wazi, shirika hilo limesema lilitaka kuwashirikisha wadau kwa kuonesha wasiwasi wake kuhusu usalama wa maji yah mto Seine lakini pia hatari zitakazowakabili wanamichezo watakaotumia maji yake.

Mamlaka za jiji la Paris ziko katika shinikizo la kukimbizana na muda kuusafisha mto huo kabla ya kuanza kwa Olimpiki Julai 26, huku njia hiyo maarufu ya maji ikitarajiwa kuwa mhimili wa michezo ya majini.

Takriban euro bilioni 1.4 (dola bilioni 1.5) zimetumika kuboresha miundombinu ya maji taka na maji mfano wa dhoruba ili kupunguza kiwango cha kinyesi kisichotibiwa kinachotiririka kwenye mto huo.

Hata hivyo mamlaka zimetupilia mbali ripoti hii mpya zikisema maji yam to huo yanaelekea kuwa salama kwa binadamu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.