Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yashambulia 'miundombinu muhimu' katika mkoa wa Kharkiv (gavana)

Vikosi vya Urusi vimefanya angalau mashambulizi 10 usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi dhidi ya "miundombinu muhimu" katika mkoa wa Kharkiv, kaskazini mashariki mwa Ukraine, gavana wa mkoa huo ametangaza leo Alhamisi asubuhi.

Waokoaji wakifanya kazi katika eneo la mashambulizi ya anga ya Urusi, huku kukiwa na shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, katika kijiji cha Lyptsi, katika mkoa wa Kharkiv, Ukraine Aprili 10, 2024.
Waokoaji wakifanya kazi katika eneo la mashambulizi ya anga ya Urusi, huku kukiwa na shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, katika kijiji cha Lyptsi, katika mkoa wa Kharkiv, Ukraine Aprili 10, 2024. REUTERS - Volodymyr Pavlov
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na chapisho kwenye Telegramu na Meya wa Kharkiv Igor Terekhov, jeshi la Urusi limeshambulia jiji hilo la pili kwa watu wengi nchini Ukraine kwa "makombora".

"Kwa kuzingatia kile mchokozi ambaye ni Urusi analenga, shida za usambazaji wa nishati zinawezekana huko Kharkiv. Usafiri wa treni za mwendo kasi utasitishwa kwa saa chache zijazo, hivyo pangeni safari zenu ipasavyo, Bw. Terekhov, meya wa Kharkiv, ameandika kwenye mtandao wa kijamii siku ya Alhamisi asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.