Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Mkuu wa polisi Aden aponea chupuchupu

Mlipuaji wa kujitoa mhanga alimlenga Kamanda Mkuu polisi mjini Aden nchini Yemen, wakati ambapo hali ya usalam inaripotiwa kudororakila kukicha.

Wanajeshi wakipiga doria katika kata ya Mansoura mjini Aden, Machi 30, 2016.
Wanajeshi wakipiga doria katika kata ya Mansoura mjini Aden, Machi 30, 2016. REUTERS/Fawaz Salman
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa Jenerali Shallal Shayae aliponea shambulizi hilo lakini mlinzi wake alijeruhiwa baada ya shambulizi hilo kulenga makaazi yake.

Mtu mmoja aliyeshuhudia shambulizi hilo amesema, mlipuaji huyo alikuwa amevalia mavazi ya kike na alionekana akisimama katika ukuta unaozunguka nyumba ya Kamanda huyo wa polisi.

Serikali ya Yemen imeendelea kupambana na waasi wa Kihuthi wanaotaka kuipindua serikali iliyo madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.