Pata taarifa kuu
UN yajipanga kuzuia mauaji ya kimbari yasirudi kutokea

UN yajipanga kuzuia mauaji ya kimbari yasirudi kutokea

Umoja wa mataifa UN unasema kuwa mauaji ya halaiki yanaweza kuzuiliwa yasitokee tena kwa utolewaji wa taarifa, wananchi kuhamasishwa, kuwa na ujasiri pamoja na utashi wa kisiasa.

Askari wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka Ghana akifuata jinsi wakimbizi kutoa jamii ya watutsi wakihamishwa mjini Kigali, juni 20 mwaka 1994.
Askari wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka Ghana akifuata jinsi wakimbizi kutoa jamii ya watutsi wakihamishwa mjini Kigali, juni 20 mwaka 1994. AFP
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari kwenye ofisi za UN hapo jana, naibu katibu mkuu Jan Eliasson amesema ni lazima jumuiya ya kimataifa ijifunze kutokana na kile kilichotokea nchini Rwanda na kuhakikisha kuwa matukio kama haya hayajirudii katika karne hii.

Colin Keating aliwahi kuwa balozi wa New Zealand kwenye Umoja wa Mataifa na hapo jana alikuwa rais wa kikao cha baraza la usalama.

Katika hatua nyingine nchi ya Ufaransa imependekeza kufanyika kwa uchunguzi wa kimataifa kuhusu tuhuma kuwa taifa hilo lilihusika kwenye kuchochea mauaji ya watutsi na wahutu ambapo watu zaidi ya laki 8 walipoteza maisha.

Hubert Vedrine, ambaye alikuwa katibu mkuu kiongozi kwenye ikulu ya Ufransa wakati mauaji haya ya kimbari yakitokea nchini Rwanda, amesema tuhuma dhidi ya Ufaransa kwa kuihusisha katika mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda, hazina msingi.

“Tuhuma za serikali ya Kigali dhidi ya operesheni “TURQUOISE” ni kashfa tupu, na pia kwa sababu mahakimu wanadai kuthibitisha kuwa Ufaransa imeshiriki na kuwa imeficha mambo mengi kwenye nyaraka zake bila ya kujali jitihada zilizofanyika kuweka wazi nyaraka hizo na siri za taifa kwa ajili ya upekuzi, lakini pia wanaozungumzia nyaraka hawazungumzii nyaraka za marekani, Ubelgiji Uganda na RPF, huu ni mkakati kwa kututuhumu”, amesema Vedrine.

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa wakijadili kuhusu namna ya kuzuia mauwaji ya kimbari yasirudi kutokea.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa wakijadili kuhusu namna ya kuzuia mauwaji ya kimbari yasirudi kutokea. REUTERS/Eduardo Munoz

Kumbukumbu hii inafanyika kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ikiwa imepita wiki moja tu toka wananchi wa Rwanda waadhimishe juma moja la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea miaka 20 iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.