Pata taarifa kuu
NIGERIA-Usalama

Nigeria: watu 18 wauwa katika shambulio la bomu mjini Abuja

Watu 18 wamepoteza maisha na zaidi ya 80 wamejeruhiwa baada ya bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari dogo kulipuka katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, Idara ya shughuli za uokozi imethibitisha.

Kituo cha magari cha Nyanya mjini Abuja, kinaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya mabomu.
Kituo cha magari cha Nyanya mjini Abuja, kinaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya mabomu. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo umetokea saa mbili saa za kimataifa usiku wa jana katika ktuo cha magari cha Nyanya, kwenye umbali wa mita 50 na eneo kulikotokea mlipuko mwengine aprili 14, shambulio liliodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kislamu wa kundi la Boko Haram, ambalo liliwaua watu 75 na makumi wengine kujeruhiwa.

Watu 75 waliuawa katika mashambulizi mawili mfululizo yaliyotokea aprili 14 mwaka 2014 katika kituo cha magari cha Nyanya kusini mwa mji wa Abuja,nchini Nigeria.
Watu 75 waliuawa katika mashambulizi mawili mfululizo yaliyotokea aprili 14 mwaka 2014 katika kituo cha magari cha Nyanya kusini mwa mji wa Abuja,nchini Nigeria. EUTERS/Afolabi Sotunde

Mashahidi wanasema, shambulio hilo liliwalenga maafisa wa polisi waliokuwa wanalinda kizuizi cha kuingia katika kituo hicho cha mabasi.
Hadi sasa hakuna kundi lililojitokeza na kudai kutekeleza shambulio hilo, lakini mwezi uliopita kundi la wanamgambo wa kislamu la Boko Haram lilikiri kushmabulia kituo hicho cha mabasi.

Kutokea kwa mashambulizi haya jijini Abuja, kumeanza kuzua wasiwasi wa kundi hilo lenye makaazi yake kaskazini mwa nchi hiyo , ambalo limeanza kuulenga mji mkuu wa taifa hilo.

Shamabulio hili linakuja juma moja kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa kiuchumi, mjini Abuja na polisi wanasema watahakikisha kuwa wageni wanakuwa katika salama thabiti.

Wanaharakati wa vyama vya kiraia wakiandamana kwa kushinikiza jeshi na polisi kufanya liwezekanalo ili wasichana waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram waachiwe huru.
Wanaharakati wa vyama vya kiraia wakiandamana kwa kushinikiza jeshi na polisi kufanya liwezekanalo ili wasichana waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram waachiwe huru. Reuters/Afolabi Sotunde

Mbali na hilo jeshi nchini humo limeendelea kuwatafuta zaidi ya wasichana 200 waliotkewa nyara na watu wasiojulikana wakiwa shuleni mwezi uliopita katika jimbo la Borno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.