Pata taarifa kuu
FDLR-MONUSCO-DRC

Wapiganaji wa FDLR wasema wataendelea kujisalimisha zaidi mwezi huu

Kundi la pili la wapiganaji wenye asili ya Rwanda wanaotuhumiwa kuhusika na mauji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini mwao, juma hili wamesema watajisalimisha kwa hiari yao kwenye tume ya Umoja wa Mataifa, kiongozi wa kundi hilo amethibitisha.

Sehemu ya wapiganaji wa kundi la FDLR ambalo limesema wapiganaji wake wataendelea kujisalimisha
Sehemu ya wapiganaji wa kundi la FDLR ambalo limesema wapiganaji wake wataendelea kujisalimisha Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wa kihutu wa FDLR juma moja lililopita kundi la kwanza lilisalimisha silaha na kujisalimisha mbele ya viongozi wa tume ya Umoja huo MUNUSCO na sasa wanasema kuwa tarehe 9 ya mwezi June mwaka huu watajisalimisha tena.

Kundi la The Democratic Forces for the Liberation of Rwanda FDLR linatuhumiwa na Umoja wa Mataifa kwa kuhusika moja kwa moja na mauaji ya Watutsi zaidi ya laki nane nchini mwao wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.

Reddition de militants du FDLR, à Kateku, dans l'est de la RDC, le 30 mai 2014.
Reddition de militants du FDLR, à Kateku, dans l'est de la RDC, le 30 mai 2014. REUTERS/Kenny Katombe

Zaidi ya wapiganai wa FDLR mia moja walijisalimisha kwa hiari yao Ijumaa ya wiki iliyopita kwenye jimbo la Kivu Kaskazini ambapo walisalimisha pia silaha zao, huku gavana wa jimbo hilo akiwapa muda kuchagua iwapo watarejea nchini mwao ama wataomba hifadhi nchini DRC.

Katibu mtendaji wa muda wa kundi la FDLR, Wilson Irategeka, amesema kuwa sasa kundi hilo linapanga kumaliza uasi wake mashariki mwa RDC na kwamba wataendelea kujisalimisha.

Irategeka amesema kuwa tarehe 9 ya mwezi June mwaka huu kundi jingine la wapiganaji hao, watajisalimisha kwenye eneo la Kigogo kwenye jimbo la Kivu Kusini ingawa hakuweka wazi hasa ni wapiganaji wanagapi ambao watajisalimisha.

Reuters

Wapiganaji wa FDLR wamekuwa wakiishi nchini DRC kama wakimbizi toka nchini Rwanda toka vita vya mwaka 1994 na ambapo sasa kundi hilo limeendelea kudumaa na kukosa nguvu huku idadi ya wapiganaji wake ikikadiriwa kufikia 1500 wakati Serikali ya Rwanda ikisema wanakadiriwa kufikia elfu 4.

Wapiganaji hawa wametawanyika kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo la Kivu ambapo wamekuwa wakituhumiwa na Serikali ya DRC pamoja na Umoja wa Mataifa kwa kushiriki vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch, hivi karibuni lilitoa ripoti yake ya kila mwaka ikieleza namna kundi hilo lilivyotekeleza vitendo vya unyanyasaji na mauji dhidi ya raia hasa wanawake na watoto kwa kuwakata shingo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.