Pata taarifa kuu
DRC-UN

UN yaitaka Congo (DRC) kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti kuhusu hali ya ubakaji wa wanawake na unyanyasaji wa kijinsia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo zaidi ya wanawake elfu tatu walibakwa kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa kitengo cha Haki za Binadamu, Bi Navi Pillay, akitoa wito kwa serikali ya Congo kutoa kipaumbele kwa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Kamishna wa Umoja wa Mataifa kitengo cha Haki za Binadamu, Bi Navi Pillay, akitoa wito kwa serikali ya Congo kutoa kipaumbele kwa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia. REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo imeorodhesha vitendo ambavyo vimewaathiri watu wapatao 3635 nchini humo kuanzia mwezi januari mwaka 2010 hadi mwezi desemba mwaka 2013, ambao asilimia (73%) ya idadi hiyo ni wanawake.

Katika kuwasilisha ripoti hii kwa vyombo vya habari, Kamishna wa Umoja wa Mataifa kitengo cha Haki za Binadamu, Bi Navi Pillay, ametoa wito kwa serikali ya Congo kutoa kipaumbele kwa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, kukamilisha uchunguzi kwa ufanisi na uhuru na kuwafungulia mashitaka watuhumiwa wakiwemo waasi na askari wa jeshi la FARDC.

Aidha, ripoti inapendekeza pia kwamba serikali ya DRC itoe msaada wa kisheria bure kwa waathirika, kuanzisha mfuko kwa ajili yao na kupitisha sheria kuhusu ulinzi wa waathirika na mashahidi wao ambao mara nyingi wanalengwa na vitisho.

Ripoti hiyo imetolewa sanjari na kesi inayowatuhumu askari wa Congo takriban 39 kuhusika na ubakaji, mauaji na uporaji novemba mwaka 2012 mjini MINOVA mashariki mwa nchi hiyo, kesi ambayo inasikilizwa hivi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.