Pata taarifa kuu
DRC-Usalama

DRC : hali ya wasiwasi yatanda mjini Kinshasa

Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanajaribu kutoa mwanga kuhusu jaribio la watu wenye silaha, ambao walijipenyeza katika kambi ya kijeshi mjini Kinshasa, ambapo hali hio imepelekea watu kuwa na wasiwasi jana jumanne mjini Kinshasa, kabla ya hali ya utulivu kurejea jioni.

Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais wakiwa kwenye barabara iingiyayo katika kambi ya kijeshi ya Tshatshi mjini Kinshasa, baada ya shambulio la jumanne Julai 22 mwaka 2014.
Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais wakiwa kwenye barabara iingiyayo katika kambi ya kijeshi ya Tshatshi mjini Kinshasa, baada ya shambulio la jumanne Julai 22 mwaka 2014. AFP PHOTO / JUNIOR D. KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Awali viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefahamisha kwamba wamezima jaribio hilo amabalo lilipelekea milio ya risase kusikia kwa muda wa saa moja mjini Kinshasa.

Hali hio ya wasiswasi ilianza wakati wanajeshi wa kikosi cha ulizi wa rais (GR) walimiminika kwa wingi katika barabara zinazoingia na kutoka kwenye ikulu na makaazi ya rais Joseph Kabila, kaskazini mwa mji, pamoja na kwenye uwanja wa ndege wa N'djili.

Wanahabari wa shirika la habari la Ufaransa AFP walisikia milio ya risase katika kambi ya kijeshi ya Tshatshi, ambako afisa wa kikosi cha ulinzi wa rais amewaambia kwamba wanajeshi wa kikosi hicho walikua wakikabiliana na kundi la zaidi ya watu ishirini wenye silaha, ambao walifaulu kujpenya katika kambi hio.

Afisa mmoja wa kikosi cha ulizi wa rais, ambaye hakuta jina lake litajwe, amesema kwamba watu 5 wenye silaha wameuawa, lakini hakuna taarifa rasmi ziliyothibitisha kuuawa kwa watu hao.

Desemba 30 mwaka 2013, mji wa Kinshasa ulishambuliwa na watu zadi ya 30 wenye silaha, ambao walishambulia Uwanja wa ndege, makao makuu ya shirika la utangazaji nchini Congo (Rtnc) pamoja na kambi ya jeshi ya Tshatshi. Mwanga kuhusu shambulio hilo hadi leo bado haujatolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.