Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-ETHIOPIA-Mazungumzo-Mapigano-Usalama

Sudani Kusini: Mazungumzo ya amani yaahirishwa

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudani Kusini na waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa rais, Riek Machar yanaendelea kukabiliwa na kizungumkuti.

Rais Sava Kiir (kushoto) akiwa pamoja na kiongozi wa waasi Riek Machar (kulia) Mei 9 Addis Ababa.
Rais Sava Kiir (kushoto) akiwa pamoja na kiongozi wa waasi Riek Machar (kulia) Mei 9 Addis Ababa. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Ukanda wa Afrika ya Mashariki (Igad) ambayo inasimamia mazungumzo kati ya pande hizo mbili, mazungumzo hayo yameahirishwa mara kadhaa.

Mazungumzo kati ya serikali ya Sudani Kusini na waasi huenda yakaenza kwa mara nyiongine tena katikati ya mwezi Oktoba mwaka 2014. Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanalenga kurejesha hali ya utulivu katika taifa hilo changa, ambalo linakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Desemba 15 mwaka 2013.

Mazungumzo yalianza mwezi Januari mwaka 2014 katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, hadi leo hayajazaa matunda yoyote.

Jumuiya hiyo ya kikanda (Igad) inayosimamia mazungumzo hayo, imefahamisha Jumapili Oktoba 5 kwamba mazungumzo kati ya pande zinazohasimiana Sudani Kusini yameahirishwa hadi katikati ya mwezi Oktoba mwaka 2014.

Igad ina matumaini kwamba huenda pande hizo hasimu zikafikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayo washirikisha wadau wote kutoka pande hizo mbili.

Tume ya usuluhishi ya Igad imebaini katika tangazo lake kwamba wajumbe wa pande hizo mbili wamejiondoa katika mazungumzo ili kuendelea kusahuriana kati yao. Mkutano mwengine umepangwa kufanyika Oktoba 16.

Kulingana pia na IGAD, hatua kubwa imepigwa katika kikao cha hivi karibuni cha mazungumzo kati ya wajumbe kutoka pande hizo mbili ikilinganishwa na vikao vingine viliyotangulia, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.

Hata hivyo pande mbili hasimu hazikuweka wazi kuhusu uwezekano wa makubaliano ya kugawana madaraka, licha ya Igad kuonya pande hizo mbili hasimu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Hata ahadi za kusitisha mapigano hazikuheshimishwa kwa siku kadhaa.

Mapigano kati ya waasi wanaoongozwa na Riek Machar na jeshi la Sudani Kusini yamesababisha vifo vya maelfu ya raia, huku watu milioni 1.5 wakilazimika kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.