Pata taarifa kuu
AFRIKA-SOKA-MICHEZO-EBOLA-AFYA

Soka: CAF yachukua uamzi kufuatia ombi la Morocco kuhusu Ebola

Shirikisho la Soka barani Afrika CAF halina mpango wa kuahirisha michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika (CAN 2015), ambayo imepangwa kuanza Januari 17 hadi Februari, kutokana na Ebola, licha ya ombi la mwenyeji wa michuano hiyo Morocco.

Uwanja wa mpira wa Cassablanca, Septema mwaka 2014.
Uwanja wa mpira wa Cassablanca, Septema mwaka 2014. AFP PHOTO / STR
Matangazo ya kibiashara

Majadiliano kuhusu suala hilo yanapangwa kufanyikaya mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Si juu ya kanuni. Shrikisho la Soka barani Afrika limechukua msimamo huo baada ya Morocc, ambayo ni mwenyeji ya michuano hiyo mwaka 2015 kuomba michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika iahirishwe kutokana na usalama wa raia kuhusu maabukizi ya virusi vya Ebola, ambavyo vinaendelea kuathiri mataifa ya Afrika Magharibi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

“ Tangu michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika CAN ianze mwaka 1957, haijawahi kuahirishwa”, shirika hilo la Soka Afrika CAF limesema Jumamosi Oktoba 11 mwaka 2014.

Siku moja kabla , Waziri wa Vijana na Michezo wa Morocco aliandikia barua shirikisho la Soka barani Afrika CAF, akiomba michuano hiyo iahirishwe kama hatua ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya Ebola duniani.

Hayo yanajiri wakati Homa ya Ebola imesababisha vifo vya watu 4000 Afrika Magharibi, huku CAF ikibaini kwamba imechukua tahadhari za Homa hiyo ya Ebola, hususan kwa kupiga marufuku mechi ziliyokua zimepangwa kuchezwa tangu mwezi Agosti nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone, mataifa ambayo yanaendelea kuahtirika zaidi na Homa ya Ebola.

Hata hivo CAF imebaini kwamba iko tayari kwa mazungumzo kuhusu suala hilo la kuahirishwa kwa michuano ya kombe la Mataifa barani Afrika. Suala hilo litajadiliwa na kamati tendaji ya CAF Novemba 2 mjini Algiers, nchini Algeria, na baadaye Novemba 3 chini Morocco pamoja na viongozi wa Morocco.

Kuahirishwa au kufutwa kwa michuano hiyo ya Kombe la Mataifa barani Afrika itakuwa itakua ni pigo kubwa kwa CAF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.