Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Jeshi la Burkina Faso latangaza serikali ya mpito

Burkina Faso imeendelea kuwa katika hofu. Alhamisi Oktoba 30 asubuhi, wabunge wa Burkina Faso wangelijadili muswada wa sheria kuhusu marekebisho ya Katiba ili kumpa nafasi ya kugombea kwa muhula mwengine rais Blaise Compaoré.

Rais Blaise Compaoré, Julai 26 mwaka 2014 katika Ikulu ya Burkinabe.
Rais Blaise Compaoré, Julai 26 mwaka 2014 katika Ikulu ya Burkinabe. AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Muswada huo umepingwa na upinzani. Kabla ya kuanza kwa mkutano wa wabunge, waandamanaji wameweza kuingia ndani ya Bunge. Tangu wakati huo, hali ya wasiwasi ilianza iliondezeka saa baada ya saa, huku machafuko yakiripotiwa karibu na Ikulu.

Hata hivo rais Blaise Compaoré ametangaza Alhamisi jioni Oktoba 30 kwamba amevunja serikali na kutangaza kuwa nchi hiyo iko katika hali ya vita. Wakati huo huo Blaise Compaoré ameomba mazungumzo na upinzani.

Wakati huo huo mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Mohamed Ibn Chambas anasuburiwa Burkina Faso Ijumaa Oktoba 31 katika jitihada za kurejesha amani nchini humo kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika na Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi (Cédéao).

Alhamisi mchana Oktoba 30, majengo ya kituo cha televisheni ya serikali yameshambuliwa na waandamanaji, hadi kusababisha matangazo ya kituo hicho kusimama kwa muda.

Jengo la Bunge limechomwa moto, huku mtu moja akiripotiwa kuawa katika maandamano hayo, ambapo waandamanaji wamekua wakikabiliana na vikosi vya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.