Pata taarifa kuu
MALI-Ebola-Afya

Ebola: mtu mwengine afariki Mali

Muuguzi mmoja wa hospitali inayomilikiwa na mtu binafsi mjini Bamako, nchini Mali amefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola. Inasadikiwa kuwa muuguzi huyo huenda aliambukizwa virusi vya Ebola na raia kutoka Guinea aliye lazwa katika hospitali hiyo na baadaye kufariki.

Zoezi la kuwafanyia vipimo vya joto raia katika mji wa mali ulioko kwenye mpaka wa Guinea, Oktoba 2 mwaka 2014.
Zoezi la kuwafanyia vipimo vya joto raia katika mji wa mali ulioko kwenye mpaka wa Guinea, Oktoba 2 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Inadhaniwa kuwa huenda mtu huyo kutoka Guinea alikua na virusi vya Ebola. Uchunguzi umeonyesha kuwa muuguzi huyo amefariki kutokana na Ebola, licha ya kuwa viongozi nchini Mali hawajathibitisha kisa hicho.

Mtu wa kwanza kubainika kuwa na virusi vya Ebola nchini Mali alikua ni msichana mdogo, mwenye umri wa miaka miwili katika kijiji cha Kayes. Mtoto huyo aliambukizwa virusi vya Ebola akiwa Guinea, na baadae alifariki baada ya jitihada za matabibu za kuokoa maisha yake.

Usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano Novemba 12, hali ya tahadhari iliwekwa katika hospitali alipokua amelazwa muuguzi huyo. Hakuna mtu aliye kuwa akiruhusiwa kuondoka katika hospitali hiyo aidha kuingia.

Muuguzi huyo alikua na mawasiliano na raia huyo kutoka Guinea, ambaye aliruhusiwa kulazwa katika hospitali hiyo baada ya afya yake kudhohofika. Lakini baada ya siku kadhaa raia huyo wa Guinea alifariki na muili wake ulirejeshwa Guinea. Mmoja kati ya ndugu zake alifariki pia baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola miezi miwili iliyopita.

Hali ya wasiwasi imetanda katika mji wa Bamako, lakini serikali imewataka raia kuwa watulivu. Zoezi la kuwakagua watu waliyowasiliana na muuguzi huyo aliye fariki kutokana na virusi vya Ebola limeanza.

Wauguzi wa hospitali hiyo pamoja na wagonjwa waliyokua na mawasiliano ya karibu na muuguzi huyo wamewekwa karantini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.